Thursday, August 15, 2013

AMUANGUSHIA KIPIGO MKE WAKE HADI KUFA KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI



Na Steven Augustino,
Namtumbo.

MFUGAJI mmoja wa Kisukuma anayeishi katika kijiji cha Mtelamwahi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, Maiko Sajini (24) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumshushia kipigo mke wake hadi kufa.

Chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ilitokana na wivu wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo Anna Yohana ambaye ni mjomba wa marehemu alisema kuwa marehemu Dagwanedi Jogi (22) alikumbwa na mkasa huo, baada ya mumewe huyo kumtuhumu kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mmoja anayeishi kijijini hapo ambaye hakumtaja jina lake, hali ambayo ilizusha mtafaruku huo katika ya wanandoa hao.

Alisema siku ya tukio mumewe huyo alisafiri kwenda kijiji jirani na kawaida yake huwa anarudi usiku wa manane lakini anaporudi   humkuta mkewe  akiwa amelala, lakini cha kushangaza wakati akikaribia nyumbani hapo alikutana na kijana huyo njiani ambaye kila mara alidai kuwa amekuwa akimhisi kumuingilia katika ndoa yake, na hata alipofika nyumbani kwake alimkuta mkewe akiwahaja lala hali ambayo ilimfanya  amhoji juu ya hali hiyo.

Alisema wakiwa katika mahojiano hayo ilitokea kutoelewana kwa wanandoa hao, ambapo mwanaume huyo aliomba amkague mkewe katika sehemu zake za siri ili aweze kujiridhisha juu ya mashaka yake, lakini mkewe alikataa hali ambayo ilisababisha vurugu na mtuhumiwa huyo kutumia nguvu katika ukaguzi huo ambapo baada ya kuangalia aligundua kuwa mkewe huyo alikuwa ametoka kufanya mapenzi.



Akizungumzia tukio hilo mtendaji wa kata ya Ligera Alli Manoni alisema kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, yeye kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha Mtelemwahi walienda eneo la tukio na kushuhudia unyama huo lakini mtuhumiwa alikuwa amekimbia, hivyo walikwenda kutoa taarifa Polisi ambao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anaelekea katika kijiji cha Suruti wilayani Namtumbo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusdedith Nsimeki amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani, kujibu tuhuma za mauaji hayo.

Aidha Kamanda Nsimeki alifafanua kuwa Polisi wanaendelea kumsaka mtu ambaye alidai kuwa chanzo cha ugomvi huo, ambaye hadi sasa   jina lake halijafahamika.

No comments: