Tuesday, August 6, 2013

MPIRA WA PETE WAENDELEA KUSHIKA KASI WILAYANI MBINGA

Wachezaji wa mpira wa pete, wakiendelea kuonesha vipaji vyao uwanja wa michezo Mbinga mjini.



Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.


LIGI ya Nanenane ya mpira wa pete wilaya ya Mbinga mkoani  Ruvuma ikiwa inaendelea kwa kasi mjini hapa kutimua vumbi, timu mbili zimeonyesha kiwango chake cha mchezo  kwenye uwanja wa michezo Mbinga mjini.


Timu ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii [FDC] ndiyo ambayo ilikuwa ya kwanza kufungua dimba majira ya saa 8:00 mchana ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 28-4 dhidi ya Timu ya Nyoni.
   

Katika kipindi chote cha  mchezo huo timu ya Nyoni  ilionekana kuwa machachali kimchezo, lakini hadi mwisho haikuweza kuzaa matunda na ilionekana ikiwa nyuma kimagoli.


Aidha timu nyingine katika mashindano hayo ambayo ilianza kucheza majira ya saa 9:30 alasiri, Polisi ya mjini hapa iliibuka na ushindi wa mabao 15 - 5 dhidi ya wapinzani wao Bambo Invenstment ya Myangayanga.
     

Katika mchezo huo timu zote mbili  zilionekana zikiwa na nguvu sawa katika kipindi cha kwanza na kwamba timu ya Bambo Invenstment ya Myangayanga, imeonekana kuwa ikichezesha vijana wenye umri mdogo na ambayo inanizamu kimchezo  zaidi kuliko timu nyingine zote zinazoshiriki mashindano hayo, ambapo refalii Winfrida Amlani hadi alipopuliza kipenga chake cha mwisho kila timu iliibuka na ushindi wake.
  

Kwa upande wa kocha msaidizi wa timu ya Polisi na  Bambo invenstment, Mariamu Honde aliziambia timu zake kuwa zinauhakika wa kuchukua ushindi, kwa kuwa timu hizo zinaongoza kimagoli, na kwamba wanahitaji walimu tu wa kufundisha michezo hiyo hasa timu za vijijini ambazo zimeonekana kuwa nyuma sana kimchezo, na kushindwa kufuata utaratibu na kanuni husika, kuliko timu nyingine ambazo zinashiriki mashindano hayo.
   

Hata hivyo Honde aliitaka serikali wilayani hapa  itoe mafuzo ya makocha wa mpira wa pete, kwa kuwa mchezo huo umeonekana kuwa nyuma kuliko michezo mingine ambayo inachezwa katika wilaya ya Mbinga.

No comments: