Saturday, November 15, 2014

NGAGA KIBULI HIKI KWA MAMBO UNAYOYAFANYA UNAKIPATA WAPI, MBINGA UNAIPELEKA WAPI?


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

TAARIFA zilizotufikia hivi punde Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Hussein Ngaga ameitisha kikao na Waratibu elimu kata wakiwemo pia Watendaji wa kata wa wilaya hiyo kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya maendeleo husika, ikiwemo suala la waratibu hao na watendaji kwa lengo la kutaka kuwarubuni kwa namna moja au nyingine juu ya kukubalina naye katika mgogoro ambao unaendelea sasa kati yake na Afisa elimu msingi wa wilaya hiyo Mathias Mkali. 

Kikao hicho ambacho kinafanyika katika ukumbi wa Jumba la maendeleo mjini hapa, vyanzo mbalimbali vya habari vimeeleza kuwa kukutana na watu hao kunatokana na Mkurugenzi huyo kuendelea kupanga njama na kutangaza kwamba Afisa elimu huyo ni mwizi, ili watendaji hao na waratibu wamkubali kwa kile anachokitaka yeye jambo ambalo wengi wao wamekuwa wakishangazwa nalo, huku wengine wakieleza kuwa ni vyema Ngaga akaachana na mambo hayo badala yake awe mbunifu wa mambo ya kimaendeleo na sio kuendekeza migogoro isiyokuwa na tija kwa jamii.

Walisema, Mkurugenzi huyo tokea afike wilayani hapa ni mtu wa kuendekeza majungu na migogoro isiyokuwa na msingi kwa wananchi wa Mbinga, huku wakihofia kwamba endapo ataendeleza mambo hayo huenda wilaya hiyo ikarudi nyuma kimaendeleo.

Katika hatua nyingine wengi wao walieleza kuwa tokea afike katika wilaya hii ni mwaka mmoja sasa umepita, lakini amekuwa ni mtu wa kupenda migogoro na kupanga safu katika idara mbalimbali kwa lengo la kutaka kuweka wakuu wa idara ambao yeye anawataka kwa maslahi yake binafsi.

“Hivi sasa badala ya kubuni mambo ya kimaendeleo yeye amekuwa ni mtu wa kutengeneza migogoro tu na kupanga safu katika idara mbalimbali hapa wilayani, ni vyema awe mtu wa kubuni maendeleo ili wananchi wa Mbinga waweze kunufaika na matunda yake, tunachotambua serikali ilimleta hapa asimamie maendeleo sio kutengeneza fitina na migogoro ambayo sasa inaturudisha nyuma”, walisema.

Pamoja na mambo mengine walieleza kuwa wanashangazwa na hali hiyo ambayo Mkurugenzi huyo anaiendeleza, huku wakiongeza kuwa huenda yeye binafsi akawa na matatizo au upangaji huo wa safu ni mbinu za kutengeneza mianya ya kujinufaisha yeye binafsi kwa namna moja au nyingine.

Kadhalika habari zilizotufikia kutoka vyanzo mbalimbali vimeeleza kwamba Ngaga ni mtu wa kupenda kugombana na kujenga migogoro isiyokuwa ya lazima kwa wafanyakazi wenzake, kama ilivyo sasa kwa hapa Mbinga, ambapo akiwa kama Mweka hazina (DT) katika wilaya alizotoka akifanyia kazi alikuwa hata hana maelewano mazuri na viongozi wenzake, kwa mfano Halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Wengine wanasema hata Mkurugenzi aliyekuwepo awali wilayani hapa na kuahamia wilaya ya Nyasa Shaibu Nnunduma, wakati anamkataa akihamiwa kuwa DT, alikuwa na maana yake hivyo sasa wanambinga wanajionea wenyewe kwa vurugu hizi anazozifanya ambazo hazina faida kwao.

Mwandishi wa habari hizi, hivi karibuni alipomtafuta Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Hussein Ngaga ofisini kwake alisema, “mimi nasema kama unataka kwenda kuandika kaandike tu sina jambo la kusema katika hili”. 

“Hata waandishi wengine wenzako walikuja hapa, niliwaambia kama kuandika nendeni mkaandike tu mimi siogopi”, alisema Ngaga.


No comments: