Na Kassian Nyandindi,
Songea.
ALIYEKUWA Mstahiki Meya wa Halmashauri
ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Charles Mhagama katika kipindi kilichopita
ameshindwa kutetea kiti chake cha udiwani kata ya Matogoro kupitia tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa hiyo, baada ya mgombea udiwani wa kata
hiyo kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Alawi Kawelea, kuibuka mshindi.
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la
Songea, Raphael Kimari alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
alisema CCM kimefanikiwa kushinda kata 16, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kimeshinda kata 4 na CUF kimeshinda kata 1 ambapo jimbo hilo lina jumla ya kata
21.
Charles Mhagama. |
Kimari aliwataja washindi wa Chama
Cha Mapinduzi na kata zao kwenye mabano, kuwa ni Oddo Mbunda (Mjimwema), Festo
Mlelwa (Seedfarm), Mshawej Hassan (Subira), Maurus Lungu (Mletele), Yobo Mapunda
(Lilambo), Lotari Mbawala (Mshangano), Cresensia Kapinga (Ndilimalitembo) na
Osmund Kapinga wa kutoka kata ya Mwengemshindo.
Aliwataja wengine kuwa ni Wilbart
Mahundi (Ruhuwiko), Ismail Aziz (Misufini), Shaib Kitete (Mjini), Hussein
Abukadi (Majengo), George Oddo (Lizaboni), Golden Sanga (Bombambili), Izack
Lutengano (Msamala) na Mussa Mwakaja kata ya Mateka.
Msimamizi huyo alizitaja kata
ambazo CHADEMA kimeshinda kuwa ni Rashid Msuso (Ruvuma), Mussa Ndomba (Tanga),
Martin Mlata (Matarawe), Seneta Yatembo (Mfaranyaki) na Alawi Kawelea kata ya
Matogoro ambaye ameshinda kiti hicho kupitia Chama cha Wananchi CUF.
Hata hivyo alisema kwamba mpaka
sasa, hajapokea malalamiko yoyote kuhusiana na matokeo hayo na kwamba hali hiyo
inaonesha kuwa Tume ya uchaguzi imetenda haki kwa wagombea wote, na wananchi
wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua kiongozi ambaye wanamtaka.
No comments:
Post a Comment