Na Kassian Nandindi,
Songea.
ASKARI wawili wa Jeshi la magereza, gereza la mifugo la
Majimaji lililopo wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, wamefariki dunia baada ya
pikipiki waliyokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela |
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela aliwataja
askari hao waliopoteza maisha kuwa ni B 7303(Wader) Oscar Henry (29) na B 5361
CPL Geofrey Mwambigija (26) wote ni askari wa gereza hilo.
Alisema siku hiyo ya tukio, kwenye barabara inayotoka Tunduru
kwenda Masasi pikipiki isiyofahamika namba za usajili ambayo ilikuwa
ikiendeshwa na B 7303(Wader) Oscar Henry ikiwa kwenye mwendo kasi ilianguka na
kusababisha vifo vyao.
Askari hao wawili walifariki dunia, mara baada ya kufikishwa
hospitali ya wilaya Tunduru na kwamba pikipiki yao baada ya kupata ajali
iliibiwa na watu wasiofahamika, ambao walikimbia na kutokomea nayo kusikojulikana.
Pamoja na mambo mengine, alisema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi wa dereva wa pikipiki hiyo ambayo ilimfanya ashindwe kumudu usukani
na kwa hivi sasa Polisi, inaendelea kuwasaka watu walioiba pikipiki hiyo.
No comments:
Post a Comment