Na Muhidin Amri,
Namatumbo.
SERIKALI imesema,
itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wauguzi, madaktari
na kuboresha miundombinu mbalimbali ili kuwavutia watumishi wa
idara ya afya, kupenda kufanya kazi wakiwa katika mazingira mazuri na
waweze kutekeleza majukumu ya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Kauli hiyo ilitolewa
na Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Chande Nalicho alipokuwa akifungua
mkutano wa mwaka wa uchaguzi kwa viongozi wa chama cha wauguzi mkoani
humo, uliofanyika kwenye ukumbi wa Faraja uliopo mjini hapa.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Chande Nalicho. |
Alifafanua kuwa
serikali inatambua matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa idara hiyo, ambapo
itaendelea kuboresha mazingira yao ikiwemo pia mishahara na maeneo ya kufanyia
kazi zao.
Mkuu huyo wa wilaya
aliongeza kuwa bado serikali inaendelea kuajiri watumishi wengi mwaka hadi
mwaka, sambamba na ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na hospitali ili kukidhi
mahitaji husika ya watanzania kwa kila mkoa, wilaya, kata na vijiji
ikiwa ni lengo kwamba wananchi wake waweze kupata huduma ya matibabu kwa
urahisi.
Nalicho alisema kazi
ya uuguzi inahitaji moyo wa uzalendo na kujituma, hivyo watumishi
wake wanapaswa kujiangalia kuhusu utendaji wa kazi zao na kuwafichua wenzao,
ambao wanakwenda kinyume na taaluma hiyo jambo ambalo linahatarisha usalama wa
maisha ya binadamu.
Kutokana na hilo,
amewahimiza pia kutekeleza wajibu wao kwa kufuata maadili ya kazi
zao pamoja na miongozo mbalimbali iliyowekwa na Wizara ya afya na ustawi wa
jamii, kitendo ambacho kitasaidia kupunguza malalamiko ya hapa na pale kutoka
kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment