Revocatus Malimi, kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma. |
Na Muhidin Amri,
Ruvuma.
JESHI la Polisi
mkoani Ruvuma, linawashikilia watu 18 kwa kosa la kujiandikisha zaidi ya
mara mbili katika daftari la kudumu la wapiga kura, kwa njia ya
kielektroniki (BVR).
Kukamatwa kwa watu
hao, kumetokana na ushirikiano kati ya Jeshi hilo na taasisi nyingine
zinazohusika na uandikishaji huo.
Kaimu Kamanda wa
Polisi wa mkoa huo, Revocutus Malimi alisema kwamba watu hao wamekamatwa kutoka
maeneo mbalimbali ya mkoa huo, hata hivyo bado wanaendelea kuwatafuta
wengine ambao wanadaiwa nao kujiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari
hilo.
Malimi alieleza kuwa kati yao wapo watumishi wa idara ya serikali, wanafunzi, wakulima, wafanyabiashara na watu wa kawaida ambapo katika wilaya ya Songea wamekamatwa watu nane.
Wilaya ya Tunduru
watatu, ambao tayari wamefikishwa Mahakamani, wilaya ya Mbinga watu watano na Nyasa
wamekamatwa watu wawili ambao nao wamefikishwa Mahamani, kujibu mashitaka ya
kosa hilo walilolifanya.
No comments:
Post a Comment