Na Steven Augustino,
Tunduru.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya vijana wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Tunduru Kaskazini wilayani Tunduru mkoa wa
Ruvuma, wameanzisha utaratibu wa kupita nyumba kwa nyumba ili kumsaidia kufanya
kampeni mgombea ubunge, kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Manjolo
Kambili ambaye anaungwa mkono na UKAWA.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutotajwa
majina yao walisema, walisema kuwa maamuzi hayo wameyachukua baada ya kubaini
kuwa mgombea ubunge aliyeteuliwa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi,
Mhandisi Ramo Makani kuwa hawamtaki.
Walisema wamelazimika kuingia katika mapambano hayo, ili
kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa CCM, anang'olewa kupitia Sanduku la kura katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
"Sisi ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi, hatuna mpango
wa kuhama chama lakini hatumtaki Ramo", walisema.
Katika kampeni hizo walisema, wanawahamasisha wananchi wa Jimbo
hilo kumchagua mgombea wa CUF katika nafasi ya ubunge, rais na diwani.
Walisema Ramo amekuwa akikigawa chama, katika makundi
ya walionacho na wasionacho kwa ajili ya manufaa yake binafsi, na kusababisha
jimbo kupoteza viti vingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka
2014.
Katika kipindi ha uongozi wake anadaiwa kuwa miaka
mitano aliyopewa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao mwaka 2010, aliahidi kutoa
nafasi kwa mwanamke mmoja kila kijiji katika jimbo hilo kwenda kusomea
mafunzo ya ujasiriamali, na kutoa pikipiki kwa vijana waliomsaidia kampeni
lakini hai leo hii ahadi hizo hajazitekeleza.
No comments:
Post a Comment