Monday, November 19, 2012

BENKI YA DUNIA YAONYA KUHUSU HALI YA HEWA

Benki ya Dunia imeonya kwamba vipimo vya joto duniani vinaweza kuongezeka kwa alama 4 Celsius ifikapo mwisho wa karne hii, iwapo juhudi zaidi za kutunza mazingira ili kupunguza makali ya kubadilika kwa hali ya hewa hazitachukuliwa.

Ripoti ya benki hiyo imesema kuwa dunia nzima inakumbwa na kupanda kwa viwango vya bahari, ukosefu wa chakula, hali mbaya ya hewa – huku nchi maskini zikiathirika zaidi.


Inasema kuwa kuna uwezekano wa kupanda kwa kiwango cha joto kwa alama 3 Celsius, hata kama nchi zote zitafikia malengo yao ya kupunguza athari zijulikanazo kama “greenhouse”.

Rais wa benki ya dunia, Jim Yong Kim, alisema umaskini hautaangamizwa, iwapo dunia nzima haitazingatia mabadiliko ya hali ya hewa.(BBC News)

No comments: