Wednesday, November 14, 2012

VIONGOZI WAPYA KUCHAGULIWA CHINA

Chama cha Kikomunisti nchini Uchina, kinakamilisha kongamano lake, siku moja kabla ya kutaja viongozi wapya watakaoongoza nchi hiyo kwa miaka Kumi ijayo.

Mwandishi wa BBC, mjini Beijing anasema mkutano huo una mipangilio mahususi kuhakikisha hakuna lolote linaloharibika.

Hatua ya kwanza ni kwa wajumbe zaidi ya elfu mbili kuchagua kamati kuu, ambapo wanachama watakaokiongoza chama hicho, watachaguliwa.


Makamu wa rais wa Uchina, Xi Jinping, anatarajiwa na wengi kuchukua hatamu za uongozi kutoka kwa rais Hu Jintao, ambaye pia atakuwa katika kamati kuu, itakayotangazwa siku ya Alhamisi.(BBC News)

No comments: