Wednesday, November 7, 2012

DEREVA KWENYE AJALI YA MANDELA AACHILIWA

Marehemu Zenani Mandela

Dereva wa gari iliyohusika na ajali iliyomuua kitukuu wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, ameachiliwa baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na mahakama.

Wakili wa Sizwe Mankazana, alisema kuwa mteja wake alifutiliwa madai yote dhidi yake ikiwemo kuendesha gari akiwa mlevi.

Alikuwa anamrejesha nyumbani Zenani Mandela kutoka kwenye tamasha la kabla ya kuanza kwa kombe la dunia mwaka 2010 wakati gari lililokuwa limewabeba lilipogonga chuma.

Zenani alikuwa mmoja wa vitukuu tisa wa bwana Mandela.
Mandela aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika KusinI, alipigia debe sana nchi hiyo kuandaa michuano ya kombe la dunia.

Wakili wa Mankazana, Hulme Scholes, alisema kuwa mahakimu waliitaja ajali hiyo kama ya kutisha.

Bwana Mankazana alikuwa emefutiliwa mbali makosa yake ya kuendesha ovyo gari pamoja na kuwa mlevi, hali ambayo ilihatarisha maisha yake.

Nyanyake Zenani sasa anasimamia kampeini ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha kuhusu usalama barabarani.

Afrika Kusini ina mojawapo ya rekodi mbaya sana za usalama wa barabarabni, na inakadiriwa kuwa watu 42 hufariki kila siku katika barabara za nchini humo. (From BBC News)

No comments: