Obama alituma ujumbe kwenye Twitter baada ya kupata taarifa za ushindi wake akiwashukuru wapiga kura.
Hotuba
yake ya ushindi:
Rais
wa Marekani Barack Obama amechaguliwa tena kwa muhula wa pili na kumshinda
mpinzani wake wa Republican Mitt Romney.
Barack ambaye ni
rais wa kwanza mweusi wa Marekani, alipata kura 270 za (Electral College)
zilizohitajika ili kupata ushindi.
Taarifa zinazohusiana:
Kura hizi hupigwa na watu maalum wanaoteuliwa na majimbo
kulingana na idadi ya miji katika majimbo hayo.
Katika hotuba yake
ya ushindi, mbele ya umati mkubwa wa watu mjini Chicago, Obama alisema kuwa atashauriana na
bwana Romney kuhusu wanavyoweza kuendesha nchi hiyo.
Aidha Obama
aliweza kuwashawishi wananchi kumpigia kura na hivyo kushinda licha ya
changamoto nyingi zilizowavunja moyo wananchi hususan swala la uchumi.
Obama pia
alikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa mshindani wake Mit Romney.
Wabunge wake wa
Democrats waliweza kusalia na idadi yao
kubwa katika bunge la Senate ambalo wameshikilia tangu mwaka 2007.
Wabunge wa
Republican nao wataendelea kudhibiti bunge la waakilishi, hatua ambayo wadadisi
wanasema kuwa huenda likasalia kuwa kikwazo kikubwa kwa Obama na mipango yake
ya nchi hasa kuhusu maswala ya sheria.
Sherehe zilizofuata ushindi wa Barack Obama:
Katika hotuba yake
ya ushindi Obama aliwataka wapinzani wake kushirikiana naye kuleta mageuzi
nchini humo.
Zikiwa zimesalia
tu kura 29 kutoka kwa jimbo la Florida,
Obama aliweza kushinda kura 303 dhidi ya kura 206 za Mit Romney.
Katika kura za
ujumla zilizopigwa na wananchi ambazo ni muhimu kisiasa ingawa sizo ambazo
zinampa rais ushindi , ushindani mkali ulidhirika kwani Obama alipata asilima
hamsini huku Romney akipata asilimia 48.
Obama alimpongeza
bwana Romney na mgombea mwenza wake Paul Ryan kwa kuendesha kampeini yao iliyokuwa na
ushindani mkubwa.
Bwana Obama
alisema anarejea ikulu ya White house akiwa na motisha zaidi kumaliza kazi
aliyoianzisha na kuhakikisha mustakabali mwema kwa wamarekani.
Obama
alituma ujumbe kwenye Twitter baada ya kupata taarifa za ushidni wake
akiwashukuru wapiga kura
Katika hisia
zilizotolewa kote ulimwenguni kufuatia ushindi wa rais Obama, Wizara ya mambo
ya nje ya Uchina imesema rais Hu Jintao na waizri mkuu Wen Jiabao wamempongeza
Obama kuchaguliwa tena kuwa rais.
Waziri mkuu wa
Uingereza David Cameron, amesema Rais Obama amekuwa kiongozi mwenye mafanikio
na alitazamia kuendelea kufanya kazi naye.
Rais wa Umoja wa
Ulaya Herman van Rompuy, amesema ana furaha kuhusu ushindi wa rais Obama. Naye
waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema uhusiano kati ya nchi yake na
Marekani umezidi kuwa na nguvu kushinda siku za nyuma. (From BBC Swahili News)
No comments:
Post a Comment