Tuesday, November 13, 2012

KASHFA YA KAMANDA WA MAJESHI MAREKANI

Kamanda John Allen.













 
Idara ya ulinzi ya Marekani inamchunguza kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, Generali John Allen, kwa kutuma ujumbe usiostahiki wa barua pepe kwa mwanamke aliye na uhusiano na aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, David Petraeus.

Waziri wa usalama Leon Panetta anasema kuwa FBI iliwasilisha kashfa hiyo kwa wizara ya usalama siku ya Jumapili.

David Petraeus alijiuzulu siku ya Ijumaa baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake.

Bw. Panetta alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa aliomba uteuzi wa Generali Allen kuwa kamanda mkuu wa majeshi ya ushirika wa Marekani na Ulaya kucheleweshwa na kwamba Rais Obama aliitikia ombi hilo.

Aliamuru uchunguzi kufanywa dhidi ya Generali Allen siku ya Jumatatu.

Generali Allen anasemekana kumtumia barua pepe Jill Kelley, mwanamke aliyeolewa kutoka Florida. Tayari mwanamke huyo alikuwa ametajwa katika kashfa dhidi ya Petraeus baada ya kuambia FBI kuwa alipokea ujumbe wa kumdhulumu kutoka kwa watu asiowajua.

Bi Kelley inasemekana alipokea barua ya kumtisha maisha yake kutoka kwa mwanamke anayejulikana kama Paula Broadwell, mwanamke ambaye bwana Petraeus alikuwa na uhusiano naye.

Msemaji mmoja wa FBI amethibitisha kuwa maafisa waliingia katika nyumba ya familia ya Paula Broadwell, jioni, lakini hakuelezea ni kwa nini.

Anadaiwa kumtumia barua pepe za kumnyanyasa,Jill Kelley, ambaye aliwaripoti kwa rafiki yake katika FBI.

Idara hiyo ilitekeleza uchunguzi wa miezi kadhaa ambao uhusiano huo kati ya Paula Broadwell and David Petraeus ulifichuliwa.

Mshauri mmoja wa Jenerali huyo anasema Petraeus ana majuto mengi na amefedheheshwa na aibu kuhusu suala hilo.

Utata huo umeibua masuali magumu kuhusu majukumu halisi ya FBI na kwa nini Ikulu ya White House haikufahamishwa kuhusu uchunguzi huo wiki iliyopita.(BBC News)


No comments: