CHANGAMOTO:
ZOEZI la uzoaji wa taka Mbinga mjini ni jambo la busara ambalo tungependa kuliona linakuwa endelevu.
Jicho letu limeshuhudia changamoto iliyopo sasa ni kwamba wazoaji wanaofanya kazi hiyo wamekuwa wakizoa taka, bila kupewa vifaa kama vile "Gloves" utakuta wanazoa taka bila vifaa hivyo muhimu.
Ni vyema sasa uongozi husika ukachukua jukumu la kuwapa vifaa muhimu ambavyo vitakinga afya zao, zisiweze kushambuliwa na wadudu watokanao na uchafu.
Tunatambua kwamba mji wa Mbinga una mamlaka ya mji mdogo ambayo ina viongozi wa sekta mbalimbali, ikiwemo hii ya afya.
Tunachohitaji hapa ni kuona Bwana afya wa mamlaka hiyo anatekeleza majukumu yake ya kazi alizopewa, ikiwemo hili la kusimamia kazi ya kugawa vifaa vya kufanyia kazi ya uzoaji taka kwa wafanyakazi waliopewa jukumu la kufanya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment