Na
Dustan Ndunguru,
Songea.
CHAMA
cha mpira wa miguu mkoani Ruvuma(FARU) kimepata viongozi wapya watakaoongoza chama
hicho, kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Uchaguzi
wa kuwachagua viongozi hao ulifanyika kwenye ukumbi wa Walimu SACCOS Songea mjini,
ambapo mwenyekiti anayemaliza muda wake Joseph Mapunda alishindwa kutetea
nafasi yake baada ya kubwagwa chini na Golden Sanga.
Akitangaza matokeo mwenyekiti wa kamati huru ya uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu mkoani Ruvuma, ambaye pia ni katibu tawala wa wilaya ya Songea Joseph Kapinga alimtangaza Golden Sanga kuwa mwenyekiti kwa kupata kura 17 sawa na asilimia 53.13 dhidi ya Joseph Mapunda aliyepata kura 15 sawa na asilimia 46.88.
Kapinga alimtangaza Dk. Zubery Kivo kuwa makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 24 ambapo nafasi ya katibu mkuu ilinyakuliwa na Ahmad Challe baada ya kupata kura 17.
Katika nafasi ya katibu mkuu msaidizi ilichukuliwa na Ajabu
Chitete aliyepata kura 14 na kwamba Deograsias Liganga alishinda nafasi ya
mweka hazina baada ya kupata kura 29.
Nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu TFF ilinyakuliwa na Humphray
Milanzi baada ya kupata kura 24 ambapo wajumbe wa kamati tendaji ni Emmanuel Komba
aliyepata kura 24 na Kelvin Haule aliyepata kura 25 ambapo nafasi hiyo ilipaswa
kuwa na wajumbe watatu lakini walioomba kugombea walikuwa wawili.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi nafasi ya uenyekiti,
Sanga aliwataka viongozi wa wilaya na mkoa kwa ujumla kujenga ushirikiano katika
kukuza kiwango cha soka mkoani Ruvuma, na
kwamba atahakikisha anaimarisha mshikamano miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment