Waasi wa Mali. |
Muungano wa Afrika AU umeunga mkono mpango wa
kuwatuma wanajeshi wa kutunza amani nchini Mali, kusaidia katika
harakati za kupamabana na wanamgambo wa Kiislamu walioko Kaskazini mwa
nchi hiyo.
Kamati kuu wa muungano huo, imeidhinisha uamuzi uliochukuliwa na Muungano wa Kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wa kutuma wanajeshi 3,000 kusaidia serikali ya Mali, kupambana na waasi hao.
Mpango huo sasa utawasilishwa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Wapiganaji wa Kiisalmu na wa kabila la Toureq walichukua udhibiti wa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya rais wa nchi kuondolewa madarakani kufuatia mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa wapiganaji hao wa Kiislamu wanataka kutekelezwa kwa sheria kali za Kiislamu katika maeneo wanayoyathibiti.
Ripoti ya Umoja huo imesema visa vya ndoa vya lazima, vimeongezeka sawia na wasichana kulazimisha kufanya vitendo vya ukahaba na pia kesi za ubakaji zimeongezeka.
Muungano huo wa ECOWAS unatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi sita, awamu ya kwanza ikiwa mpango wa kuwapa mafunzo na kujenga kambi Kusini mwa Mali, kabla ya kuanzisha mikakati ya kijeshi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchi za Nigeria, Niger na Burkina Faso zimehaidi kutoa wanajeshi hao watakaotumwa nchini Mali.
Baada ya kuidhinisha mpango hupo, kamishna mkuu wa Usalama na Amani wa muungano wa Afrika, Ramtane Lamamra, ametoa wito kwa mataifa mengine ya kiafrika kutoa wanajeshi zaidi na misaada zaidi ili kufanikisha mpango huu.(BBC News)
No comments:
Post a Comment