MKuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu. |
Na
Dustan Ndunguru,
Tunduru.
VIJANA
wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wametakiwa
kutokata tamaa ya maisha badala yake watumie muda wao kujiendeleza
kielimu ikiwemo kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mafanikio
wanayohitaji.
Hayo
yalisemwa na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Chande Nalicho, wakati alipokuwa akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Chiwana huku akisema, kama kijana atakuwa hajapata
nafasi ya kujiendeleza kielimu ajikite katika shughuli za kimaendeleo.
Bw.
Nalicho alisema kuwa vijana wengi wamekuwa na tabia ya kukata tama, jambo
ambalo sio zuri na kwamba badala yake wanapaswa kubuni njia mbalimbali za
kujiletea maendeleo, ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa vikundi vya uzalishaji mali.
“Kutokana
na tatizo la ajira lililopo sasa ni muhimu kwa vijana kutumia akili zao wenyewe
kutafuta na kubuni njia bora za kufanya, zitakazowasaidia kujipatia mahitaji yao ya kila siku kuliko
kusubiri ajira ambazo hawana uhakika nazo, serikali imeweka mazingira mazuri
ambayo yatamwezesha kila anayewajibika kwa lolote kufanikisha”, alisema.
Alisema
ujinga na maradhi ni kichocheo kikubwa cha umasikini na kwamba hali hiyo
huchangiwa kwa kiasi kikubwa ukosefu wa elimu hivyo wakati umefika kwa wazazi
na vijana wenyewe kuanza kubadilika na kutambua umuhimu wa elimu.
Mkuu
huyo wa wilaya aliwakumbusha wananchi wa wilaya hiyo kuanza maandalizi ya msimu
mpya wa kilimo, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mwaka huu mvua zimewahi
kunyesha mapema ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
No comments:
Post a Comment