Watu wanaosadikika kuwa ni vibaka wamemuua kwa kumpiga na kitu
kizito katika paji la uso dereva boda boda eneo la National mjini
Iringa Abeli Nyunza na kumpora piki piki yake.Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika eneo la Muungano
Frelimo mjini Iringa jirani na shule ya msingi Muungano.
Wakielezea juu ya tukio hilo mashuhuda wamedai kuwa majira ya usiku walisikia mlio wa pikipiki na
ghafla ulizimika na baada ya hapo ilisikika sauti ikiita kwa nguvu
Peter ! Peter ! mfano wa mtu aliyekuwa akiomba msaada na baada ya
dakika kama 10 hivi ukimya ulitanda na ghafla ulisikika mlio wa
pikipiki ukiondoka kwa kasi.
Mwenyekiti wa boda boda mjini Iringa Bw. Macurius Chengulla mbali ya
kuthibitisha kifo cha dereva boda boda mwenzao huyo bado amesema
kuwa wameweka mkakati wa kuendesha msako ili kuwabana wahusika wa
mauwaji hayo.
Bw. Chengulla amesema kuwa matukio hayo ya kuuwawa kwa madereva boda boda
kwa Manispa ya Iringa ni tukio la kwanza kwa mwaka huu japo matukio ya
kutekwa na kujeruhiwa yamekuwa yakitokea .( Picha kwa hisani ya Francis Godwin)
|
No comments:
Post a Comment