Mkaa wa mawe.
WAHOFIA UTOROSHWAJI WA MAKAA YA MAWE:
WANANCHI wa kijiji cha Liyombo kata ya Ruanda wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameonyesha wasiwasi wao juu ya kudaiwa kutoroshwa kwa makaa ya mawe pamoja na ulipwaji wa fidia watakazo pata kwa mali zao, baada ya kufahamika kuwa kijiji hicho kimejengwa juu ya mwamba wa makaa ya mawe ambayo yanatarajiwa kuanza kuchimbwa kabla ya mwisho wa mwaka huu iwapo taratibu za vibali kwa mwekezaji zitakamilika.
Baadhi ya
wakazi wa kijiji hicho kilichopo katika kata ya Ruanda ambao ni Bw. Elia Hyera, John Mbepera na Joakimu Nchimbi wakizungumzia suala hilo wametoa
wito kwa serikali kusimamia na kuhakikisha wanalipwa fidia pamoja na kuwa
makini na kufuatilia sampuli za makaa hayo zinazopelekwa nje ya nchi kwa madai
ya kwenda kufanya utafiti wa ubora wa makaa ya mawe kabla ya kuanza kuchimbwa.
Utafiti huo ulianza April mwaka 2008 kwa kuangalia wingi wa makaa ya mawe, unene wa mwamba na ubora wa makaa hayo na sasa yanachimbwa kwa wingi.
Utafiti huo ambao
umefanyika katika kijiji hicho kwa miaka minne sasa umebaini kuwa kijiji cha
Liyombo kipo juu ya mwamba bora wa makaa ya mawe ambapo TANCOAL ina hisa ya asilimia 70.
Mgodi huo umekuwa chanzo kikubwa cha utoaji wa makaa ya mawe hapa nchini na kusambaza kwa wahitaji wote wa nishati hiyo hapa nchini, vikiwemo viwanda na nje ya nchi na kwamba kitakuwa chanzo kikuu cha umeme kimataifa na msaada katika gridi ya umeme ya taifa ambayo hivi sasa umeme wake hautoshelezi na kusababisha makali ya umeme mgawo.
Mtaalamu wa miamba Bw.
Alex Sostenes anasema makaa hayo ya mawe yamesambaa
maeneo yote ya Ngaka na Liyombo pamoja na maeneo mengine ya jirani
na kijiji cha Liyombo na kwamba mashine ya utafiti kwa utalaamu imetoboa shimo
moja kijijini hapo ili kubaini wingi wa mkaa na ubora wake na kuwataka
wanakijiji wasiwe na wasiwasi juu ya nyumba zao ama mali zao.
Hata hivyo
mkurugenzi mkuu wa TANCOAL Bw. Emmanuel Costantinides amethibitisha
kuwa mkaa wa mawe wa kijiji cha Liyombo ni mkaa bora kutokana na majibu
ya “ sampuri zilizopelekwa Afrika Kusini kwa uchunguzi kupitia Bandari ya
Ndumbi Ziwa Nyasa.
“Kiasi cha tani
1000 zilisafirishwa kupelekewa nchini Afrika ya kusini kwa uchunguzi wa awali
kwa madhumuni ya kujiridhisha ambapo matokeo yameonyesha dalili nzuri kuwa
mkaa unaonyesha ubora wake haufanani na mkaa wa mawe unaochimbwa katika
nchi yeyote duniani, mkaa wa Mbinga ni bora kuliko mikaa mingine yote duniani’’, alisisitiza.
Alisema tani 10,000 zinahitajika kupelekwa nchini Afrika ya kusini kama sampuri kutoka eneo la utafiti ili wanunuzi waweze kujiridhisha zaidi ingawa hali hiyo inaleta hofu kwa wakazi wa kijiji hicho, ambao wanashauri ni bora utafiti ungefanyika hapa hapa nchini ili kusifanyike hujuma ya kusafirisha maliasili kama hii, nje ya nchi kwa kisingizio cha utafiti huku watanzania wakibakia kuambulia mashimo kutokana na uharibifu wa mazingira.
Mgodi wa makaa ya
mawe ya Liyombo na Ngaka wilayani Mbinga umekadiriwa kuwa na zaidi ya
tani 400 milioni za mkaa wa mawe. Kiasi hicho kwa mujibu wa wataalam, kinaweza
kuchimbwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.
Sera Taifa ya madini ya mwaka 1997 inasisitiza juu ya sekta binafsi kuendeleza madini, na wakati huo huo Serikali ikiwa na jukumu la kuidhibiti, kuikuza, kuiwezesha na kuiendelea. Sekta ya madini inachangia takribani asilimia 2.3 ya pato la Taifa, ambayo inakadiriwa kufikia asilimia 10 ifikapo 2025. (Posted by Jicho letu nuru ya jamii)
No comments:
Post a Comment