TAARIFA YA UCHUNGUZI WA KIFO CHA MWANDISHI WA
HABARI WA CHANNEL TEN BW. DAUD MWANGOSI:
1.0 UTANGULIZI:
Mnamo tarehe 03 Septemba mwaka 2012, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (MB) aliteua Kamati ya
watu watano kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwandishi wa habari wa
kituo cha televisheni cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi,
kilichotokea tarehe 02 Septemba 2012, katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya
Mufindi, Mkoa wa Iringa. Kituo cha kazi cha marehemu Daud Mwangosi kilikuwa
mkoa wa Iringa ambapo pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
Habari wa Mkoa wa Iringa (IPC).
Wajumbe wa Kamati hiyo ni:
Jaji (Mst.) Steven Ihema – Mwenyekiti
Bibi Pili Mtambalike – Mjumbe
Kanali (Dkt. Eng) Wema Wilson Wekwe – Mjumbe
Bwana Theophil Makunga – Mjumbe
Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Juma. Mngulu –
Katibu
Sekretarieti ya Kamati ni:
Bi. Edith T. Assenga – Wizara ya Mambo ya
Ndani
Bwana Nasoro H. Msumi – Wizara ya Mambo ya
Ndani
2.0 HADIDU ZA REJEA:
Kamati ilipewa Hadidu za rejea zifuatazo:
- Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa na CHADEMA
eneo la Nyololo,Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba, 2012 na
kuwepo kwa uvunjifu wa amani.
- Kama
yalikuwepo makubaliano au maelekezo kuhusu mikutano ya hadhara au maandamano
nchini katika kipindi cha Sensa.
-Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi
kutumia nguvu iliyosababisha kifo cha Marehemu Daud Mwangosi na wengine
kuumizwa, na uwiano wa nguvu hiyo na tukio.
-Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la
Polisi na Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha
kuna madai ya kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi
limepanga kuwashughulikia.
-Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu zinazotoa
uwezo kwa Jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama vya Siasa na
Mamlaka ya Rufaa endapo vyama hivyo havitaridhika na amri hizo.
-Hali ya Mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na vyama vya Siasa nchini katika Utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.
3.0 MUDA WA UCHUNGUZI:
Kamati ilipewa muda wa siku 19 kuanzia tarehe
11 Septemba 2012 iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha Ripoti yake ifikapo
tarehe 02 Oktoba 2012.
4.0 NJIA ZILIZOTUMIKA KUFANYA UCHUNGUZI:
4.1 Mahojiano na watu mbalimbali waliokuwepo
kwenye tukio.
4.2 Kupitia nyaraka na vielelezo mbalimbali.
4.3 Kutembelea eneo la tukio.
4.4 Majadiliano na vikundi mbalimbali
(viongozi wa dini ngazi ya kijiji na wilaya hadi ya mkoa; viongozi wa vyama vya
siasa kwenye ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa na Taifa, viongozi wa serikali ngazi
ya kijiji, wilaya, mkoa, Taifa) na wanakijiji wa Nyololo.
5.0 UCHUNGUZI:
Kamati ya Uchunguzi ilifanya mahojiano na watu
mbalimbali ikiwa pamoja na watendaji wa serikali hususan Kamati za Ulinzi na
Usalama ngazi ya wilaya Mufindi na mkoa wa Iringa viongozi wa Jeshi la Polisi
viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Waandishi wa Habari
na wananchi wa kawaida (ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa).
6.0. YALIYOJITOKEZA:
Baada ya Kamati kukutana na makundi ya watu
mbalimbali katika Mkoa wa Iringa na Viongozi wa Vyama vya Siasa wa kitaifa
jijini Dar es Salaam, mambo kadhaa yalijitokeza
na baadhi yao
ni:
-Hofu ya kutoweka kwa amani miongoni mwa
viongozi na wananchi hasa katika mikutano na maandamano ya siasa ambayo
yameanza kuota mizizi ya uvunjifu wa amani na mengine kusababisha mauaji.
Viongozi na wananchi wengi waliotoa maoni yao
mbele ya Kamati wameonyesha hofu kuwa hali hiyo isipodhibitiwa mapema inaweza
kulipeleka pabaya Taifa letu.
-Kuna walakini wa mahusiano kati ya waandishi
wa habari na Jeshi la Polisi mkoani Iringa.
-Uwepo wa utashi wa makusudi/dhati kwa
viongozi wa vyama vyote vya siasa kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya
maslahi ya vyama.
-Umuhimu wa Ushirikiano na mahusiano baina ya
vyombo vya serikali, vyama vya siasa, wanahabari na wananchi kwa ujumla badala
kuonyeshana ubabe ambao umetufikisha hapo.
- Haja ya kufanya mabadiliko ya kisheria
katika mfumo wa usimamizi na utendaji wa masuala ya siasa nchini
- Haja ya kuwa na mabadiliko ya kimfumo katika
Jeshi la Polisi badala ya ulioko sasa ambao kwa maoni ya baadhi ya watu
waliozungumza na Kamati ni wa kitaifa zaidi na kuacha serikali za mitaa bila ya
wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao.
-Kwamba nguvu kubwa inatumika na vyombo vya
dola/usalama dhidi ya raia na hivyo kupunguza imani ya jamii kwa vyombo hivyo.
-Kupungua kwa maadili/uzalendo miongoni mwa
Watanzania kuanzia viongozi hadi wananchi hususan kwenye shughuli za kisiasa.
-Haja ya kusisitiza elimu ya uraia kwa jamii
kuanzia kwa watoto hadi kwa watu wazima hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi
ili kujenga umoja wa kitaifa.
-Kuwepo kwa mikutano na maandamano ya vyama
vya siasa yasiyokuwa na kikomo.
-Muonekano wa Jeshi la Polisi mbele ya jamii.
7.0. MATOKEO YA UCHUNGUZI KUTOKANA NA HADIDU
ZA REJEA:
7.1 Kuhusu “Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa
na CHADEMA eneo la Nyololo, Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba
2012 na kuwepo uvunjifu wa amani”, uchunguzi wa Kamati umebaini yafuatayo:
Tarehe 30 Agosti 2012 CHADEMA iliandika barua,
Ofisi ya Mkuu wa Polisi
wilaya ya Mufindi kutoa taarifa kuhusu ratiba ya
mikutano ishirini na sita (26) kwenye majimbo ya Mufindi Kusini na Kaskazini
tarehe 02-03 Septemba 2012. Awali ratiba ya mikutano hiyo ilikubaliwa, lakini
baadaye siku hiyo ya tarehe 01 Septemba 2012 mikutano hiyo ilisitishwa kwa
barua Kumb. Na MFG/A.24/9/54 kutokana na kuongezwa siku za zoezi la Sensa ya
watu na Makazi hadi tarehe 08 Septemba 2012.
CHADEMA walikataa kusitisha ratiba ya mikutano
hiyo kama inavyothibitishwa na Justin Leornard
Mpotwa Katibu wa Wilaya ya Mufindi kwa barua yake Kumb. Na
CDM/M4/002/Vol.01/2012 ya tarehe 01 Septemba 2012 kuwa “pia tunaomba ieleweke
bayana kwamba kisheria shughuli zetu hazina mwingiliano na wala kuhusiana na
program iliyoongezwa ya Sensa. Kwa barua hii tunakuarifu kuwa mikutano
tuliyokutaarifu kuifanya kuanzia kesho tarehe 02 septemba 2012 itaendelea kama ilivyopangwa – CHADEMA VEMA”.
Aidha kuwepo kwa zuio la mikutano ya Siasa ya
CHADEMA Mkoani Iringa wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
linathibitishwa na Amri ya Utendaji (Operation Order) ya Kamanda wa Polisi Mkoa
(SACP Michael Kamuhanda) ya tarehe 01 Septemba 2012. Amri ya Utendaji ambayo ni
amri halali ilitolewa ili “kuzuia shughuli za Siasa (mikutano na maandamano) kipindi
cha zoezi la kitaifa la Sensa kuanzia tarehe 25 Agosti 2012 hadi 08 Septemba
2012”. Uhalali wa Amri/Zuio hili ulithibitishwa pia na Msajili wa Vyama vya
Siasa nchini katika barua yake Kumb Na. DA. 112/ 123/ 01/ 34 ya tarehe
28/08/2010 na wakati wa mahojiano na Kamati ya uchunguzi tarehe 22 Septemba
2012.
Licha ya zuio/amri hii Viongozi wa CHADEMA
walikataa kutii amri hiyo. Kutokana na taarifa hizi, Kamati ya Uchunguzi
inathibitisha kwamba hapakuwepo na uhalali wa mkusanyiko/mkutano ulioitishwa na
CHADEMA eneo la Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba
2012. Kuhusu kuwepo kwa uvunjifu wa amani Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba
2012 Kamati ya Uchunguzi ilibaini mambo yafuatayo:
-Tukio la kuuawa kwa Daud Mwangosi jioni ya
tarehe 02 Septemba 2012 lilitokea baada ya Operesheni ya Jeshi la Polisi
kumalizika. Hii ni kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,
Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa na Joseph Senga Mpiga
picha/Mwandishi Tanzania
Daima.
- Kitendo cha kutotii amri halali ya Kamanda
wa Polisi kuagiza wafuasi wa CHADEMA watawanyike kutoka kwenye eneo la ofisi ya
Kata ya CHADEMA ilikuwa chanzo cha vurugu.
Uamuzi wa CHADEMA kung’ang’ana kukusanyika
isivyo halali eneo la Nyololo ikizingatiwa kuwepo kwa ujumbe wa SMS kutoka kwa
Dkt. Slaa, Katibu wa CHADEMA uliosema, “IGP nasubiri simu yako. Wajulishe
Polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha. Mtakuwa na karamu ya
mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Den Hague. Ni
afadhali tufe kuliko manyanyaso haya”. Dr. Slaa. : ujumbe huu ukiashiria
umwagaji wa damu ni ushaidi tosha kuwepo kwa uvunjifu wa amani. CHADEMA ndiyo
Chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba
2012.
7.2 Kama
yalikuwepo makubaliano kuhusu mikutano ya hadhara au maandamano nchini katika
kipindi cha Sensa. Katika kuzungumzia hoja hii tukianzia na Uongozi wa Serikali
na Vyama vya Siasa ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa, Kamati ya Uchunguzi
ilithibitisha kuwepo kwa maagizo ya kusimamisha mikutano/maandamano ya Vyama
vya Siasa wakati wa kipindi cha Sensa ya Watu na Makazi yaliyotolewa na Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, na kuongezwa muda wa Sensa hadi tarehe 08 Septemba
2012 na Kamishna wa Sensa hapo tarehe 01 Septemba 2012.
Aidha hoja hii imethibitika kwamba Msajili wa
Vyama vya Siasa nchini kwa barua yake yenye Kumb Na DA. 112/ 01/ 34 ya terehe
28 Agosti 2012 kwenda kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa akiwasihi
kusimamisha shughuli zote za mikutano na maandamano ya Vyama vyao kwa kipindi
chote cha Sensa ya Watu na Makazi. Aidha kwa mujibu wa Gazeti la Serikali Na 29
VOL 93 ya tarehe 20 Julai 2012, Mhe. Rais, JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa mamlaka
aliyopewa chini ya kifungu namba 14 cha Sheria ya Takwimu sura 351 alielekeza
kwamba Sensa ya Watu na Makazi itafanyika kuanzia tarehe 26 mwezi wa nane,
mpaka tarehe 08 mwezi wa tisa mwaka 2012.
Kamishna wa Sensa aliratibu zoezi la Sensa ya
Watu na Makazi kumalizika ifikapo tarehe 01 Septemba 2012. Hata hivyo kutokana
na tathmini aliyofanya, kazi hiyo ilikuwa imekamilika kwa asilimia 95%. Hivyo
tarehe 01 Septemba 2012 alitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kwamba ili kila
mwananchi apate nafasi ya kuhesabiwa watu watakaokuwa wamesalia ambao ni chini
ya 5% wanaombwa kutoa ushirikiano ili zoezi hili likamilike. Hivyo, wale wote
mmoja mmoja waliobakia wataendelea kuandikishwa hadi tarehe 08 Septemba 2012.
Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi
kwa ujumbe wa simu Kumb Na S8.7/ 2/ A/ VOL XIV/ 59 ya tarehe 28/08/2012, pia
simu yake Kumb Na C.28/ B/ 44 ya terehe 01/ 09/ 2012 aliwaelekeza Makamanda wa
Polisi wa
Mikoa kutoruhusu mikutano na maandamano wakati huu wa zoezi la Sensa
ya Watu na Makazi mpaka litakapokamilika tarehe 08 Septemba 2012.
Kimsingi Kamati ya uchunguzi imethibitisha
kwamba maelekezo kwa Vyama vya Siasa kutoendesha shughuli za mikutano ya
hadhara au maandamano yalitolewa kwa mujibu wa Sheria.
7.3 Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi
kutumia nguvu iliyosababisha, kifo cha marehemu Daud Mwangosi na wengine

Hoja kuwa Polisi walitumia nguvu kubwa katika
kudhibiti mkutano wa CHADEMA iliungwa mkono na Viongozi wa Serikali ya Kijiji,
Viongozi wa dini na Viongozi wa siasa Kijijini Wilayani na Mkoani pamoja na
Waandishi wa Habari. Hata hivyo Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya na Mkoa na
Viongozi wa Jeshi la Polisi waliona nguvu hizo ni za mazingira ya hali
ilivyokuwa.
Uchunguzi wa suala hili umebaini kwamba tarehe
02 Septemba 2012 muda wa saa 10 za jioni huko eneo la Sokoni, Kijiji cha
Nyololo kulikuwepo na mkutano usio halali ulioandaliwa na viongozi wa CHADEMA.
Upo ukweli kwamba uongozi wa Polisi ulitoa ilani kuamuru wafuasi wa CHADEMA
waliokuwepo mkutanoni hapo waondoke la sivyo nguvu itatumika. Walikaidi amri
hiyo na ilipoagizwa viongozi wakamatwe ndipo walianza kurusha mawe kwa Askari
Polisi. Baadhi ya Askari walijeruhiwa, akiwamo G 9934 PC Mgaka alivunjwa mkono
wa kulia. Pia kofia (helmet) tatu ziliharibiwa.
Kutokana na hali hiyo amri ya kupiga mabomu ya
machozi na ya kishindo ilitolewa, kwa mujibu wa Kifungu 77 hadi 79 cha Kanuni
za Adhabu, Sura ya 16 – R.E 2002. Operesheni hii ilimalizika baada ya kukamatwa
viongozi na wafuasi wa CHADEMA jumla yao
saba.
Baada ya zoezi hilo kukamilika Askari Polisi walioshiriki
kwenye Operesheni waliamriwa kuingia katika magari tayari kwa kuondoka. Wakati
Askari wakipanda kwenye magari kishindo kikubwa kilitokea umbali wa zaidi ya
mita 100 kutoka sehemu ambayo operesheni ilikuwa inafanyika na iligundulika
kwamba kishindo kile kimesababisha kifo cha Mwandishi wa Habari Daud Mwangosi.
Upelelezi wa awali pamoja na picha za mnato
unaonyesha kwamba marehemu alikuwa amemkumbatia Mkuu wa Polisi Kituo cha
Mafinga ASP Assel Mwampamba na huku akiwa amezungukwa na Askari Polisi
wasiopungua sita ambao licha ya kumzunguka marehemu Daud Mwangosi kuna madai
yaliyotolewa na mwandishi wa Habari Joseph Senga kwamba, Askari Polisi hao
walikuwa wanamshambulia marehemu kwa kumpiga, ndipo askari mmoja aliyetambuliwa
kuwa ni G 2573 PC Pasificus Cleophace Simon alifyatua Bomu la kishindo na
kusababisha kifo cha Daud Mwangosi.
Tukio hili linaweza kugawanyika katika sehemu
mbili: sehemu ya kwanza ni wileamapamebas(mni ya kutawanya watu na ya pili ni
ile ya mauaji ya Daud Picha Namba 15: Askari Polisi wakimpiga Marehemu Daud
Mwangosi, huku OCS M wenye kifimbo) akijaribu kuwazuia. Mwangosi. Katika tukio
la kwanza idadi ya Askari walioshiriki ni Sekisheni Tukio hili linaweza
kugawanyika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ni lile ya Operesheni ya
kutawanya watu na ya pili ni ile ya mauaji ya Daud Mwangosi.
Katika tukio la kwanza idadi ya Askari
walioshiriki ni Sekisheni tatu ambapo ni askari wasiozidi thelathini. Kwa
maelezo yaliyotolewa na Mwandishi wa Habari mbele ya Kamati, Bw Joseph Senga
anaeleza kuwa watu walishatawanyika na hali kutulia mara baada ya Operesheni
hii kukamilika na Polisi kujiandaa kuondoka kwenye eneo la tukio. Tukio la
mauaji ya Daud Mwangosi lilisababishwa na kupigwa bomu la kishindo.
Maswali ya kujiuliza katika tukio la mauaji ni
Je, kulikuwepo na uwiano unaolingana na tukio hili?, Je Palikuwa na uhalali wa
kutumia Bomu la kishindo?, na Je, utumiaji wa Bomu hilo ulikuwa na umuhimu?
Kulingana na tukio lenyewe majibu ya maswali
hayo ni kama ifuatavyo:
-Hapakuwa na uwiano wa Bomu na tukio la
mauaji, kwa vile utaratibu wa matumizi ya bomu hilo unaelekeza kulenga juu
usawa wa nyuzi 45 na umbali mita 80 mpaka mita 100.
-Hapakuwa na uhalali wa kutumia Bomu la Kishindo kwani lengo la ulipuaji wake ni ili watu
waogope na kukimbia.
- Hapakuwepo umuhimu wa kutumia Bomu la Kishindo kwa sababu hata ingekuwa ukamataji
tayari Askari Polisi wapatao sita walikuwepo eneo la tukio.
Kwa misingi hiyo Kamati imeona kwamba nguvu
iliyotumika mwanzo hadi kumaliza Operesheni haikuwa kubwa. Kuhusu tukio la
kuuawa Bw. Daud Mwangosi na kuumizwa baadhi ya Askari Polisi halikustahili
kabisa.
7.4 Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la
Polisi na Waandishi wa Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha madai ya
kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi limepanga
kuwashughulikia.
Katika kupata ukweli wa jambo hili, Kamati
ilikutana na wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa na pia iliwahoji
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Upelelezi wa
Mkoa, Nyigesa Ramadhani Wankyo na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani
Iringa Said Abdallah Mnunka.
Pia, wakati Kamati inakutana na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa, ilileta suala la mahusiano kati ya Polisi na
waandishi wa habari na watendaji wakuu wa serikali wa mkoa wa Iringa.
Katika mkutano na waandishi wa habari,
ilionekana kuwa katika thathmini yao uhusiano
kati yao na Polisi hapo mkoani ni mbaya sana. Walieleza matukio
kadhaa ya kunyanyaswa waandishi wa habari wakati wapo kazini, ikiwamo kupigwa,
kutishiwa kuharibiwa na kuharibiwa vifaa vyao vya kazi na hata kutishiwa maisha
ili wasiripoti mambo ambayo Polisi wana maslahi nayo.
Kwa mfano, mwandishi wa habari wa Star TV,
Oliver Moto alieleza Kamati kuwa: “Waandishi wa habari hawana mahusiano mazuri
na Jeshi la Polisi, na hata wanapofika ofisi za Polisi huwa hawapewi
ushirikiano. Kutokana na uhusiano mbaya wanahabari walifanya maandamano tarehe
06 Machi 2012 kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na Jeshi la Polisi hapa Iringa”.
Mwandishi mwingine wa habari Zulfa Shomari
ambaye anaandikia gazeti la Mwananchi alieleza kuwa kuna matukio kadhaa ambayo
Polisi wamewazuia waandishi kufanya kazi zao mojawapo ni lile ambalo Polisi
walikataza kupigwa picha tukio la kukamatwa kwa pembe za ndovu.
Kamati pia iielezwa na mwandishi wa habari wa
ITV, Bw. Laurian Mkumbata mkasa wa kuvunjwa kamera yake na OCD Iringa kwenye
tukio moja. Ilibidi OCD alipe kamera hiyo kwa maagizo ya RPC.
Pia walisema kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa
hivi sasa ana mawasiliano duni sana na waandishi wa habari na juhudi za wengi
wao kumfuata ili athibitishe tukio zimekuwa zikishindwa kwani ameweka maagizo
getini kuwa mtu yeyote ambae anataka kumuona ni lazima aeleze anataka kumuona
kwa sababu gani ndipo aruhusiwe kuingia. Kwa sababu hii waandishi wa habari
wengi wamekata mguu kwenda ofisini kwake.
Mwandishi mmoja wa Ebony FM Bw. Raymond
Francis, aliiambia Kamati kuwa yeye binafsi alitishiwa kuuawa na baada ya
kuandaa kipindi kuhusiana na watu wanaoshukiwa kufanya biashara haramu ya madawa
ya kulevya ambao wanahusiana na baadhi ya Polisi wasio waadilifu.
Mwandishi wa Habari Greyson Mgoi wa
gazeti la Kwanza Jamii aliiambia Kamati kuna tukio la kuanguka kwa lori la
mafuta eneo la Ifunda karibu na Mafinga ambapo waliwakuta wananchi na polisi
wakichota mafuta kutoka kwenye hilo
gari.
Alisema kuwa waliamua kupiga picha tukio hilo lakini Polisi
waliwakamata na kuwalazimisha wafute hizo picha walizopiga. Kwa kuogopa shari
walikubali kuzifuta na wakaruhusiwa kuendelea na safari yao.
Waandishi wa Habari hata hivyo walibainisha
kuwa uhusiano wao na Polisi hapo mkoani ulikuwa mzuri sana kipindi cha uongozi wa RPC Advocate
Nyombi. Walisema kuwa wakati wa RPC Nyombi, alikuwa na utaratibu wa kukutana na
waandishi wa habari na pia alikuwa anafikiwa na waandishi wa habari kwa urahisi
kwa simu au ofisini kwake. Walisema lakini ulianza kuharibika alipohama na
nafasi yake kuchukuliwa na RPC Mangara na kuwa mbaya zaidi alipokuja Kamuhanda.
Walidai kuwa Polisi wa Iringa si waadilifu na wamekuwa wakijiona kama miungu watu.
Waandishi walieleza Kamati, kitu kilichowaudhi
sana ni yale
majibu yaliyotolewa na RPC baada ya mauaji ya Daud Mwangosi ambayo yalionekana
yalikuwa ni ya kupanga ili ukweli usijulikane. Walisema kama si picha
zilizotolewa na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye tukio, hawadhani kama
umma wa Watanzania wangepata ukweli wa tukio hilo.
Walisema tarehe 06 Machi 2012, walifanya
maandamano ili kupinga manyanyaso ya Polisi wa mkoani Iringa yaliyopokelewa na
Mkuu wa Mkoa.
Waandishi wa Habari mkoani Iringa pia walionyesha masikitiko yao kuwa tangu kutokee kwa mauji ya Daud Mwangosi,
hawajapokea pole kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na watendaji wake wa juu hata kama ni ya “kinafiki”.
Kwa upande wa pili, yaani Jeshi la Polisi,
Kamati ilipata taswira tofauti. RPC Kamuhanda alisema kuwa yeye anaona
mahusiano ya Polisi na waandishi wa habari kwa ujumla ni mzuri na yeye binafsi
amekuwa akikutana na waandishi wa habari takriban kila siku asubuhi saa nne
kuwapa habari. Pia aliiambia Kamati kuwa waandishi wa habari walishiriki
kikamilifu katika kuripoti michuano ya mpira ya Kikombe cha Kamuhanda
yaliyofanyika mjini Iringa.
Msimamo huo pia ulichukuliwa na viongozi wa
juu wa kiutawala akiwemo Mkuu wa mkoa Dkt. Christine Ishengoma, Katibu Tawala
wa Mkoa Bibi Getrude Mpaka ambao walisema kuwa hapakuwa na uhasama wowote kati
ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa Habari. Wote wawili walisema kuwa
walimfahamu marehemu Daud Mwangosi na aliteuliwa katika kamati kadhaa za kimkoa
ikiwa ni pamoja na ile ya kuandaa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani, Kamati ya
Masuala ya Katiba ya Mkoa na Kamati ya Kukuza Utalii ya Mkoa.
Kuhusiana na hisia kuwa Mkuu wa Mkoa na
watendaji wake hawakujumuika na waandishi katika msiba wa Daud Mwangosi, Dkt.
Ishengoma alisema si kweli hawajatoa rambirambi zao kwa kifo cha Mwangosi
lakini alitoa pole kwa waandishi wakati ameenda na IGP Mwema kijijini Nyololo
na pia kupitia radio katika kipindi kilichotayarishwa na mwandishi wa habari
Francis Godwin.
Baada ya kuongea na pande hizo mbili, Kamati
imebaini kwamba kuna walakini wa mahusiano kati ya waandishi wa habari na
baadhi ya askari polisi mkoani Iringa. Kuhusu madai ya kuwepo kwa orodha ya
waandishi watatu (3) ambao jeshi la polisi limepanga kuwashughulikia.
Kwenye tukio la Nyololo ambapo mwandishi wa
habari Daud Mwangosi aliuawa, mwandishi wa habari mwengine Godfrey Mushi
alipigwa na Polisi na inasemekana kujeruhiwa vibaya na baadaye kukamatwa na
Polisi.
Kwa mujibu wa Joseph Senga mpiga
picha/mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima ambaye alikuwepo kwenye
tukio na kupiga picha, alimuona marehemu akipita nyuma ya gari moja la Polisi
ambalo lilikuwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA. Punde tu alimwona mtu
amezungurukwa na askari akipigwa lakini hakujua ni nani na yeye aliendelea
kupiga picha tukio hilo mpaka nae alipokamatwa
na Polisi watatu ambao walimwuliza kama nae
anataka aende kuungana na mtu anayepigwa pale.
Senga alisema wakati kipigo kinaendelea, kuna
askari mmoja mwenye nyota tatu (OCS Mwampamba) aliteremka kutoka kwenye gari na
kwenda pale ambapo Yule mtu aliyekuwa anapigwa huku akiwaambia “mwachieni,
mwachieni, namfahamu mimi huyo ni mwandishi wa habari!”
Senga alisema mara alisikia kishindo kikubwa
na wale askari ambao walikuwa wanamshikilia walikimbia ndipo yeye akaendelea
kupiga picha sasa za marehemu Daud Mwangosi ambaye alikuwa amekwisha
sambaratishwa na bomu. Alieleza kuwa alimsikia yule askari ambaye alikuja
kumsaidia marehemu Mwangosi akisema “afande wameniuwa”, “afande wameniuwa”,
akimwambia RPC ambaye alikuwa karibu nae kwani nae aliumizwa vibaya katika
mlipuko huo. Senga aliiambia Kamati wale wote ambao walikuwa wame mzunguka
marehemu kama wanavyoonekana kwenye picha
alizopiga walikuwepo wakati anapigwa.
Maelezo ya Bw. Senga yanatofautiana sana na yale yaliyotolewa
na RPC na OC FFU kuwa Marehemu alimvamia OCS Mwampamba na kuwa wale askari
huenda walidhania kuwa mkubwa wao alikuwa amevamiwa ndipo walipoamua kwenda
kumsaidia. OCS Mwampamba mwenyewe wakati akihojiwa na Kamati ilipokuwa Mafinga
alisema hakumbuki kitu.
Hata hivyo, kwa maelezo ya Bw. Senga, ambayo
yanakubaliana na yale ya RPC na OC-FFU, kitendo cha kupigwa na mauaji ya
marehemu Daud Mwangosi kilitokea baada ya kuisha ile operesheni ya
kusambaratisha mkutano wa CHADEMA na hapakuwa na mabishano yeyote au
purukushani iliyotokea kabla ya marehemu kuzungukwa na kuanza kupigwa.
Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa
kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa
nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?
Kwa nini kuna maelezo yanayokinzana kati ya
Bw. Senga ambaye alikuwa karibu sana na tukio na yale ya RPC na OC-FFU ambao
katika maelezo yao kwa Kamati walisema kuwa wao walikuwa mbali kidogo na tukio
kwa hiyo hawakuweza kuona kwa dhahiri kilichotokea. Maelezeo ambayo yalirudiwa
na viongozi wa juu wa Polisi ikiwa ni pamoja na Kamishna wa Upelelezi (DCI)
Robert Manumba na Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema katika mahojiano na
Kamati.
Uchunguzi wa Kamati haukuweza kupata ushahidi
wa kubainisha kama kupigwa kwa waandishi hao
kulitokana na njama yeyote ya Polisi kuwashughulikia au ilitokea kwenye
purukushani ya vurugu zilizotokea baada ya FFU kuamriwa kutawanya wanachama wa
CHADEMA.
Pia Kamati haikupata ushahidi wowote wa
kuonyesha kuwa mauaji ya Daud Mwangosi yalikuwa ni ya kupangwa. Kutokana na
maelezo ya hapo juu,
Kamati inapendekeza yafuatayo:-
-Taasisi za habari zinazosimamia maadili na
weledi wa vyombo vya habari, hususan Baraza la Habari Tanzania na
Jukwaa la Wahariri wafanye utaratibu unaostahiki za upatanishi kati ya
waandishi wa habari, Jeshi la Polisi na uongozi wa mkoa wa Iringa. Hii
itasaidia kurejesha uhusiano mzuri kati ya vyombo hivyo muhimu katika mkoa;
-Waandishi wa habari wapewe mafunzo ya jinsi
ya kuripoti matukio ya hatari/ghasia;
-Waandishi wa habari wavae vivazi maalum vya
kuwatambulisha wakiwa katika matukio hasa kwenye maeneo hatarishi;
- Waandishi wa habari wafanye kazi kwa weledi,
uadilifu, uwazi na wasijibainishe na vyama vya siasa;
- Polisi ambao walihusika katika kumpiga
marehemu Daud Mwangosi kabla hajauawa wachukuliwe hatua stahiki za kisheria;
- Kamati ya Ushirikiano kati ya Jeshi la
Polisi na Waandishi wa Habari iliyoanzishwa mwaka 2008 ifufuliwe. Na kamati
hizo ziteremke hadi kwenye ngazi ya mkoa kama
ilivyokuwa awali.
- Viongozi wa polisi wanapotoa taarifa za
tukio, ziwe zimefanyiwa utafiti wa kina ili zisipotoshe jamii.
7.5 Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu
zinazotoa uwezo kwa Jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama
vya Siasa na Mamlaka ya Rufaa ambapo vyama hivyo havitaridhika na amri hiyo.
Sheria Namba 5 ya 1992 kama
ilivyorekebishwa na Sheria Namba 7 ya 2009 inaratibu mahusiano ya kiutendaji
kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa. Kwa mujibu wa Sheria hii Jeshi la
Polisi limepewa madaraka ya kutoa zuio kwa maandishi na kuweka bayana sababu za
kuzuia mikutano au maandamano. Zuio aina hii ni halali kwa mujibu wa Sheria na
ni sherti Chama cha Siasa kiheshimu na kutii. Fungu la 11 vifungu vidogo Na 1,
4, 5, 6, 7 na 8 ya Sheria ya Vyama vya Siasa likisomwa pamoja na mafungu Namba
43, 44, 45 na 46 ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Auxiliary Forces Act Sura 322
vitatumika kusimamia uendeshaji mikutano ya Vyama vya Siasa ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Pamoja na kwamba Vyama vya Siasa
vinatakiwa kutoa taarifa na siyo kuomba idhini, Jeshi la Polisi limepewa uwezo
na madaraka juu ya mikutano hiyo kuhusu kuzuia au kuruhusu na au kutoa
maelekezo stahiki, kama vile kupendekeza, na
kushauri eneo mbadala na tarehe tofauti ya kufanya mikutano/maandamano.
Aidha kutotii amri/zuio ya Jeshi la Polisi ni
kosa la Jinai kwa mujibu wa Fungu la 74 la Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16
RE.
Vilevile kwa mujibu wa Fungu la 43 (6) ya
Sheria ya Jeshi la Polisi na Auxiliary Forces Act, Waziri wa Mambo ya Ndani
ndiye Mamlaka ya Rufaa dhidi ya amri/zuio linatolewa na Jeshi la Polisi.
Pamoja na kuwepo kwa Sheria hizi mbili bado
kuna mapungufu katika uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Siasa kwa Msajili
wa Vyama vya Siasa. Kwa mfano pamoja na madaraka aliyonayo Msajili wa Vyama vya
Siasa ya kukifuta Chama cha Siasa kwenye rejesta ya usajili kwa mujibu wa Fungu
la 19 na 20 ya Sheria ya Vyama vya Siasa, kusimamisha utoaji wa ruzuku na
matumizi yake, uratibu wa shughuli za vyama hivyo hauko mikononi mwake.
Wadau wanashauri umuhimu wa kuimarisha
uhusiano katika shughuli za utendaji kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa na Jeshi la Polisi ili kudumisha utulivu na amani na utii wa sheria bila
shuruti kwa upande mmoja na kukuza mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa
kwa upande mwingine.
7.6 Hali ya mahusiano kati ya Jeshi la Polisi
na Vyama vya Siasa nchini katika utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.
Kamati ya Uchunguzi wa Kifo cha Mwandishi wa
Habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi katika kupata majibu kwa hadidu hii ya
rejea, ilizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kutoka ngazi za Kijiji cha
Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa na Viongozi wa kitaifa jijini Dar es
Salaam na viongozi wa dini kutoka ngazi za Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya
Mufindi na Mkoa wa Iringa.
Kwa ujumla, kila kiongozi wa chama cha siasa
wa ngazi zote ambaye Kamati imezungumza naye kuhusu hadidu hii ya rejea,
ameelezea umuhimu wa Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao
na wangependa jeshi hilo liachwe huru katika kutekeleza majukumu yake bila ya
kuingiliwa na wanasiasa ili lifanye kazi zake kwa weledi na uadilifu.
Hata hivyo taswira iliyojitokeza ni kwamba
kuna mgawanyiko wa mtizamo kuhusu jinsi Jeshi la Polisi linavyoshughulikia
mikutano/maandamano ya Vyama vya Siasa.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani
wanaamini kuwa Jeshi la Polisi linakipendelea Chama cha Mapinduzi na kubinya
vyama vya upinzani, huku viongozi wa CCM kutoka ngazi ya kijiji hadi Taifa
wakilisifia Jeshi hilo
kuwa linafanya kazi yake vizuri na kwa weledi mkubwa.
Mgawanyiko wa taswira kuhusu madai kuwa Jeshi
la Polisi kuipendelea CCM hauko tu kati ya vyama vya upinzani na CCM bali pia
kwa viongozi wa dini kuanzia ngazi za kijiji, wilaya hadi mkoani Iringa kwa
maelezo kuwa hawajasikia hata siku moja mtu anauawa na Polisi kwenye mkutano wa
CCM. Mwandishi mmoja alitoa udadisi wake kuwa huwa wanapata shida sana kuandika habari za
mikutano ya CHADEMA kutokana na jinsi Polisi wanavyojipanga kwenye mikutano ya
chama hicho.
Kudhihirisha umuhimu wa Jeshi la Polisi katika
jamii, hata wale wanaolituhumu kuwa linakipendelea CCM, katika kutoa maoni yao kuhusu hatua za kuchukuliwa askari wanaoharibu sifa ya
Jeshi hilo, wanapendekeza kuwa askari wahusika
wachukuliwe hatua na kuomba Jeshi hilo
liendeshwe kwa weledi hasa inapotokea askari akalazimika kutumia silaha
kukabiliana na fujo isifikie kuua.
Kwa mfano, Mchungaji Peter Katanga wa Revival
Baptist Church, alishauri chombo cha Polisi kisitumike kufanya mauaji, au
kisitumike na mtu, watu, au kikundi chochote kufanya matendo yasiyo mazuri kwa
jamii kwa sababu chombo hicho kipo kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wote na
mali zao.
Viongozi wa siasa wengine bila kujali itikadi
zao, wameonekana kukerwa sana
na tabia ya watu kuuawa wakati Jeshi la Polisi linatuliza ghasia na hii ikiachiwa
iendelee inaweza kuleta uvunjifu wa amani katika nchi. Kwa mfano, Mchungaji wa
Kanisa la EFATA Nyololo, Mkombozi Kiliwa alishauri Polisi watumie njia
zinazofaa kukabiliana na wanaovunja sheria na si kuua.
Pia Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyololo, Obby Kimbale,
alielezea kutokukubaliana kwake na kitendo cha mauaji ya Daud Mwangosi,
alipendekeza elimu ya uraia itolewe kwa jamii nzima vikiwemo vyombo vya dola,
viongozi wa serikali, wanasiasa na wananchi kwa ujumla wao ili kila mtu kwa
nafasi yake akaelewa namna ya kutimiza wajibu wake ndani ya mfumo wa demokrasia
ya vyama vingi.
Kwa upande mwingine, wengi waliotoa maoni yao juu ya mahusiano ya
Polisi na vyama vya siasa, pamoja na kulaumu Jeshi la Polisi kutumia nguvu
kubwa katika kukabiliana na wafuasi wa CHADEMA, pia waliwalaumu viongozi wa
chama hicho, kwa kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi hatimaye kusababisha
Polisi kutumia nguvu kiasi hicho.
Kitendo cha kuuawa kwa Mwandishi wa Habari,
Daud Mwangosi na tabia ya kutokea mauaji katika mikutano ya CHADEMA kimeonekana
kuwakera viongozi wengi wa vyama vya siasa kwani wanaamini kuwa Polisi huwa
wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi ‘wanapotuliza ghasia’ katika mikutano ya
CHADEMA.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa, Zakaria
Mwansasu alielezea sababu ya matukio ya namna hii kuwa ni kutokana na
mmomonyoko aliouita mkubwa wa maadili hasa katika vyama vya siasa na akashauri
viongozi wa vyama vya siasa wakapewa elimu ya uraia.
Maoni mengi ya viongozi wa vyama vya siasa
yamejikita zaidi katika hofu ya nchi kuingia kwenye vurugu na kutoka kwenye
kisiwa cha amani na hivyo kutoa uashauri kwa viongozi wa vyama vya siasa na
Jeshi la Polisi kuweka mbele maslahi ya taifa.
Mchungaji Yokonia Koko wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), alielezea ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari
Polisi kuwa umetokana na jeshi hilo kuajiri vijana ambao hawana maadili na
kwamba watuhumiwa wa mauaji kwenye matukio yanayolihusisha Jeshi la Polisi
wakati wa kuzuia fujo katika mikutano/maandamano ya vyama vya siasa wachukuliwe
hatua kali ili iwe fundisho kwa askari wengine.
Kasi ya CHADEMA kuendesha mikutano katika
sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kujiimarisha kichama, imepokewa kwa hisia
tofauti na vyama vingine vya siasa. Wakati kuna makundi ya watu katika jamii
wakidhani kuwa hiyo ni haki yao kama chama cha siasa kinachotaka kukua na kukubalika
kisiasa, wengine wanaiona mikutano hiyo ya hadhara ya CHADEMA kama ni
kuwapunguzia muda wa kufanya shughuli zao za maendeleo hasa baada ya kipindi
cha uchaguzi kumalizika.
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, alishauri
kufanyiwa marekebisho kwenye sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992
itakayoweka wazi shughuli za vyama vya siasa baada ya Uchaguzi Mkuu.
Alisisitiza kuwa shughuli za siasa baada ya Uchaguzi Mkuu zihamie bungeni kwa
wanasiasa kuhoji mipango ya maendeleo ya serikali na matumizi ya rasilimali za
nchi na wananchi waachwe wachape kazi zao za maendeleo.
Kuhusu Jeshi la Polisi, Mukama alisema mfumo
uliopo wa Jeshi hilo unalifanya lionekane la
kitaifa zaidi na kushauri libadilishwe kimuundo ili liweze kutandaa hadi
serikali za mitaa kuongeza nguvu katika mpango wa ulinzi shirikishi
ulioanzishwa na Jeshi hilo.
Mwanasiasa John Shibuda alizungumzia mahusiano
kati ya vyama vya siasa na Jeshi la Polisi kwa kutoa lawama kwa vyama vya siasa
kuwa havitoi malezi kwa wanachama wake ambayo yatawafanya wawe waadilifu,
wazalendo, waaminifu na watiifu wa sheria.
Alisema vyama vya siasa havina mfumo wa
kujihakiki, kujikosoa na kujiwajibisha na akapendekeza kuanzishwa kwa mfumo huo
kisheria ambao utawajibisha vyama vya siasa kwa matendo ya viongozi au
wanachama wao.
Shibuda alifafanua kwamba sheria
anayopendekeza iwe na nguvu ya kutoa adhabu kwa chama cha siasa na kwa kiongozi
au mwanachama ambaye atathibitika kuwa ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.
Kuhusu Jeshi la Polisi mwanasiasa huyo
alipendekeza kufanyike kwa marekebisho ya utendaji ili wakuu wa wilaya na mikoa
waondolewe nguvu za kiutawala ambazo huwafanya wakati mwingine kutoa maagizo ya
kisiasa kwa Jeshi la Polisi na hatimaye kulifanya Jeshi hilo lionekane linatekeleza maslahi ya
wanasiasa badala ya kuwa chombo cha kulinda amani.
Kwa ujumla Kamati kutokana na maelezo
mbalimbali ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi, imeona kuwa kuna
mahusiano hafifu kati ya baadhi ya Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi.
Kwa kuwa taasisi zote hizi ni wadau muhimu wa
amani na utulivu nchini, Kamati inapendekeza:
-Kuwe na jukwaa la mazungumzo ya mara kwa mara
kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa ili kila upande ujue wajibu wake na
wa taasisi nyingine katika kudumisha amani ya nchi na utamaduni wa kuheshimu
sheria zilizopo na kupunguza migongano.
-Kuhusu madai kwamba mauaji yanayotokea nchini
yaundiwe Tume, Kamati imeona kuwa zipo sheria zinazotoa mamlaka ya kutafiti au
kuchunguza endapo kuna mashaka ya kifo hicho.
-Muundo uliopo wa Jeshi la Polisi uangaliwe
upya kisheria ili kuziba mianya inayotoa nafasi kwa wanasiasa kulitumia Jeshi hilo kwa manufaa ya
kisiasa.
-Nafasi za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa
kiutendaji ziangaliwe upya ili zisitumike na mhusika kwa ajili ya manufaa ya
kisiasa.
-Kwa kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwa
ndiye mlinzi wa usalama wa raia na mali zao, siasa za ubabe kwa vyama
vya siasa ziepukwe kwa kuwa zinaleta msuguano usio wa lazima na Jeshi la Polisi
8.0. MAONI NA MAPENDEKEZO:
Kutokana na uchunguzi uliofanyika kupitia
mahojiano na Viongozi wa kada mbalimbali, kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya, Mkoa
hadi Taifa, Kamati ina maoni na mapendekezo yafuatayo:
MAONI:

yaundiwe tume, Kamati imeona kuwa zipo sheria zinazotoa mamlaka ya kutafiti au

-Kuhusu operesheni ya uzuiaji wa mkutano wa
CHADEMA usio halali Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012, Jeshi la Polisi
lilitekeleza wajibu wake ipasavyo na kutumia nguvu sahihi. Operesheni
iliyoandaliwa na kufanyika ilikamilika kwa kuwatawanya watu waliofika kwenye
mkutano, kukamata baadhi ya Viongozi na wafuasi wa CHADEMA na hali ya utulivu
ilirejea kwenye eneo husika.
MAPENDEKEZO:
-Mauaji ya mwandishi wa habari Daud Mwangosi
yalitokea baada ya operesheni kumalizika, na amri ya kuondoka kwa askari eneo
la tukio kutolewa na Viongozi wa operesheni hiyo
-Jamii wakiwemo Viongozi waelimishwe umuhimu
wa utii wa sheria, kanuni na taratibu ili kudumisha amani na utulivu hapa
nchini. Viongozi wengi walionyesha hofu ya kuliingiza Taifa kwenye machafuko
makubwa na uvunjifu wa amani iwapo jamii haitazingatia umuhimu wa kutii sheria,
kanuni, taratibu na amri halali za Mamlaka.
-Msajili wa Vyama vya siasa afafanue majukumu
ya vikundi vya Ulinzi vya Vyama vya Siasa kama
vile Green Guard, Red Brigade, Blue Guard.
-Iwepo programu mahususi ya Elimu ya Uraia
nchini ili kujenga uzalendo na kukuza maadili ndani ya jamii wakiwemo viongozi
wa kada mbalimbali. Hivi sasa jamii inashuhudia kutoweka kwa uzalendo na kuwepo
kwa mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii.
Njia zifuatazo zitumike:
- Elimu ya uraia iimarishwe katika mitaala ya
elimu kuanzia Shule za msingi hadi Vyuo Vikuu.
- Uamuzi wa kurudisha mafunzo ya Jeshi la
Kujenga Taifa kwa vijana utekelezwe mapema.
- Vyama vya Siasa, Madhehebu ya Dini, Tasnia
ya Habari na Taasisi zisizokuwa za Serikali zishiriki kikamilifu katika uenezi
wa Elimu ya Uraia nchini.
- Kuhimiza uzingatiaji wa weledi katika
utendaji kazi kwa mujibu wa taaluma na miongozo inayotolewa kuleta ufanisi.
Aidha elimu endelevu sehemu za kazi itiliwe mkazo.
-Kufanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya
Siasa Na. 5 ya 1992 ili kuweka wazi shughuli za Vyama vya Siasa baada ya
Uchaguzi Mkuu. Lengo ni kuwa Shughuli za Siasa zihamie Bungeni kujadili na
kuhoji mipango ya Serikali na matumizi ya rasilimali za nchi. Kwa kufanya hivyo
wananchi watapata nafasi kufanya kazi za maendeleo.
-Kuboresha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, hususan uanzishwaji wa ofisi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuratibu
ushirikiano/mahusiano baina ya serikali (Jeshi la Polisi) na Vyama vya Siasa.
Lengo ni kukuza mahusiano na kuondoa mgongano.
-Utaratibu wa kufanya mikutano mara kwa mara
kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na Waandishi wa
Habari uimarishwe ili kujenga mahusiano mazuri na kupata ufumbuzi wa haraka kwa
matatizo yaliyojitokeza.
- Jeshi la Polisi nchini ni chombo muhimu
katika ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Muundo uliopo wa Jeshi la
Polisi uangaliwe upya Kisheria ili kuziba mianya inayotoa nafasi kwa wanasiasa
kulitumia Jeshi hilo
kwa manufaa ya Kisiasa. Aidha mipango ya kuboresha utendaji kazi kitaaluma
iliyopo hivi sasa upewe msukumo stahiki hususan rasilimali watu na fedha.
- Wananchi wahamasishwe kushirikiana na Polisi
Jamii na Ulinzi shirikishi. Polis ishirikiane na Serikali za mitaa kufanikisha
malengo hayo.
- Jeshi la Polisi liimarishwe ili litekeleze
majukumu yake kikamilifu na kujenga mahusiano sahihi kati yake na Jamii, Vyama
vya Siasa, Tasnia ya Habari na Asasi zisizo za Kiserikali.

Jukwaa la Wahariri wafanye utaratibu unaostahiki wa upatanishi kati ya

itasaidia kurejesha uhusiano mzuri kati ya vyombo hivyo muhimu katika mkoa.

ya kuripoti matukio ya hatari/ghasia.

kuwatambulisha wakiwa katika matukio hasa kwenye maeneo hatarishi.
-Waandishi wa habari wafanye kazi kwa weledi,
uadilifu, uwazi na wasijibainishe na vyama vya siasa.
-Kamati ya Ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi
na Waandishi wa Habari iliyoanzishwa mwaka 2008 ifufuliwe. Na kamati hizo
ziteremke hadi kwenye ngazi ya mkoa kama
ilivyokuwa awali.
-Viongozi wa Polisi wanapotoa taarifa za

9.0. CHANGAMOTO
Changamoto zilizojitokeza katika Uchunguzi
zimegawanyika katika mtiririko ufuatao:-
9.1 Jeshi la Polisi:
- Ukosefu wa Mafunzo endelevu.
- Ukosefu wa Uvumilivu katika utekelezaji wa
Majukumu.
-Uelewa mdogo wa Elimu ya Uraia.
- Mmomonyoko wa Maadili.
- Kukosekana kwa uzalendo.
- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na
Taratibu
9.2 Vyama vya Siasa:
- Kukosekana kwa uvumilivu katika kuendesha
shughuli za Siasa.
-Kukosekana kwa Elimu ya Uraia
- Uelewa mdogo wa baadhi ya Viongozi wa Vyama
kuhusu uendeshaji wa Vyama vya Siasa.
- Ukosefu wa Sera/Mwongozo kwa Vyama vya Siasa
kuendesha shughuli za Kisiasa baada ya uchaguzi mkuu.
- Kukosekana kwa Jukwaa linalokutanisha mara
kwa mara Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi
- Mmomonyoko wa Maadili.
- Suala la Uzalendo.
- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na
Taratibu
9.3 Jamii:
- Elimu ya Uraia.
- Mmomonyoko wa Maadili.
- Kukosekana kwa uzalendo.
- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na
Taratibu.
10.4 HITIMISHO:
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
wakati wa uhai wake aliwahi kusema kuwa, “ili nchi iendelee inahitaji vitu
vinne ambavyo ni watu, ardhi, siasa safi
na uongozi bora. Watanzania kila mtu mahali pake, tunahitaji kuwa na siasa safi yenye kujenga
ustawi, tija, mshikamano, amani, maendeleo na afya kwa taifa letu”.
Utulivu na amani kwa ajili ya mustakabali wa
taifa, imekuwa ni kauli mbiu ya viongozi mbalimbali ambao Kamati hii imepata
fursa ya kuzungumzia juu ya hali ya siasa na mahusiano yaliyopo baina ya Serikali,
(Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama wilaya na mkoa), vyama vya siasa,
viongozi wa dini na wananchi.
Wananchi na Viongozi wanataka kuona shughuli
za siasa ya vyama vingi inaendeshwa kwa hoja zenye tija badala ya vurugu na
utengano. Njia mojawapo ya kukabilia1.0 UTANGULIZI:
na na hali hii inayojitokeza ni kujenga
uzalendo, maadili mema, na mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha
amani na utulivu.

utengano. Njia mojawapo ya kukabiliana na hali hii inayojitokeza ni kujenga
uzalendo, maadili mema, na mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha
amani na utulivu.
Kamati hii inashauri na kupendekeza kuwa maoni
haya yazingatiwe na kutekelezwa.
Aidha Kamati imefaidika sana kupata fursa ya kukutana na viongozi
mbalimbali kuanzia kijiji hadi taifa na walitoa ushirikiano wa dhati katika
kutoa mchango wao wa mawazo. Kamati inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi (Mb) kwa imani yake kwa
wajumbe wa Kamati ya Uchuguzi. (By Iringa yetu bolg)

No comments:
Post a Comment