Viongozi wa Ufaransa na
Ujerumani wamesema kuwa wana shaka ikiwa makubaliano yaliyofikiwa kuhusu
bajeti ijayo ya muungano wa ulaya katika mkutano wa EU unaoendelea.
Rais wa ufaransa Francois Holland na Chancella wa Ujeruamani, Angela Merkel walisema hayo baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huo ambao ulifanyika saa tatu baada ya muda uliotarajiwa kutokana na tofauti zilizokuwepo kuhusu mipango ya bajeti.
Mazungumzo hayo yameahairishwa hadi baadaye alasiri hivi leo.
Mapema rais wa baraza la muungano huo wa ulaya Herman Van Rompuy, alisambaza mapendekezo yaliyofanyiwa mabadiliko ya bajeti mpya na kusema kuwa anaamini kutakuwa na masikizano.(BBC News)
No comments:
Post a Comment