Waendesha mashtaka wa kijeshi wa
Marekani wanataka hukumu ya kifo kutolewa kwa mwanajeshi mmoja
anayetuhumiwa kuwaua raia kumi na sita, wakiwemo watoto tisa, Kusini mwa
Afghanistan, mnamo mwezi Machi mwaka huu.
Baadhi ya wanajeshi wamekiambia kikao cha kesi hiyo jinsi Sajenti Robert Bales, alirejea kambini akiwa amelowa damu huku mashahidi wa Afghanistan, wakisimulia alivyofatua risasi kiholela.
Mawakili wa upande wa mshtakiwa hata hivyo wanasema hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mteja wao.
Uamuzi wa iwapo kesi kamili ya mahakama ya kijeshi itaendelea itatolewa na mojawapo wa majenerali wakuu wa jeshi la Marekani.
Hakuna mwanajeshi yoyote wa marekani amehukumiwa kifo katika miaka hamsini iliyopita. (BBC News)
No comments:
Post a Comment