Rais Mursi wa Misri anapingwa kwa kujilimbikizia madaraka |
WAANDAMANAJI wamekesha usiku kucha katika medani ya Tahrir mjini Cairo kuelezea hasira zao dhidi ya tangazo la rais wao anayezingatia itikadi za kiislamu Mohammed Morsi kujipatia madaraka makubwa.
Walikesha wakiimba nyimbo za kumlaani rais pamoja na vuguvugu lake la kiislamu la Muslim Brotherhood.
Maandamano mengine ya kumpinga rais Morsi yamefanyika katika maeneo mbali mbali nchini humo.
Bwana Morsi amejaribu kumaliza mzozo huo kwa kuahidi kuwa madaraka yake yatakuwa na kikomo.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood, ambalo bwana Mursi ni mwanachama, liliakhirisha mkutano wao siku ya Jumanne likisema linataka kuzuia taharuki kutanda miongoni mwa wanachi.
Waandamanaji wanasema Rais na chama chake cha Muslim Brotherhood wanajipatia mamlaka kinyume na sheria
Wanaomuunga mkono bwana Mursi wanasema kuwa sheria hiyo inahitajika ili kulinda mafanakio yaliyotokana na mapinduzi ya kiraia dhidi ya utawala wa Mubaraka na idara ya mahakama ambayo ilikuwa na watu wanaomuunga mkono rais aliyeng'olewa madarakani.
Waandamanaji wanasema kuwa vuguvugu la Muslim Brotherhood limeyateka nyara faida zilizotokana na mapinduzi ya kiraia.(BBC News)
No comments:
Post a Comment