Monday, November 19, 2012

MAELFU YA RAIA DRC WAWATOROKA WAASI

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo wanasema kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuzorota, huku makumi ya maelfu ya wananchi wakizidi kuwatoroka waasi.

Waasi wa M23 sasa wako kilomita chache tu kutoka mji mkuu wa mkoa wa Goma, hata baada ya kushambuliwa kwa helikopta za Umoja wa Mataifa.

Waasi hao wanasema kwamba hawakusudii kuuteka mji huo, lakini wakazi wanahofia kwamba mji huo utatekwa wakati wowote.


Inasemekana kwamba baadhi ya wanajeshi wa Kongo waliokuwa wanailinda Goma wameshatoroka.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba hautajibu mashambulizi ya waasi iwapo wataingia katika maeneo waishimo watu wengi, kwa kuhofia kuwajeruhi raia.

Kieran Dwyer, msemaji wa walinda amani hao, alisema, “Kwa sasa walinda amani wanajitahidi kuuthibiti mji wa Monigi, kilomita chache kutoka Goma, na vilevile kujaribu kuwalinda watu wengi waliotoroka – tunahisi kuwa takriban watu 60,000 wamefurushswa na mapigano haya.”(BBC News)

No comments: