Na Mwandishi wetu,
MAMLAKA ya mapato Tanzania(TRA)
mkoani Ruvuma imefanikiwa kukusanya kiasi cha
shilingi milioni 424.2 kupitia mtandao wa utoaji leseni za udereva, katika
kipindi cha mwaka 2011 hadi 2012.
Meneja
wa mamlaka ya mapato wa mkoa huo Bw. Apili Mbaruku alisema hayo alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusiana na maadhimisho ya siku ya mlipa
kodi ambapo kimkoa yanafanyika mjini Songea.
Bw. Mbaruku alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kilipatikana
kutokana na utoaji wa leseni hizo, kwa watumiaji wa vyombo vya moto ikiwemo
magari na Pikipiki.
“Katika
kipindi hicho leseni mpya 8,500 zilitolewa na bado tunaendela kufanya
mipango ya utoaji elimu kwa watu ambao hawajapata leseni hizo, ili hatimaye
waweze kuhamasika kuzipata”, alisema.
Aidha
meneja huyo alisema kwamba katika kipindi hicho mamlaka hiyo iliweza kuboresha
mfumo wa ukusanyaji kodi kwa njia ya vitalu(Block management system) ambapo
waliandikishwa walipa kodi 1,094.
Hata
hivyo katika kipindi cha mwaka 2011/2012 mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoani
Ruvuma, iliweza kukusanya shilingi bilioni 5.476 na kuvuka lengo walilopangiwa
ambapo katika msimu wa mwaka 2012/2013 wamepangiwa kukusanya kiasi cha shilingi
bilioni saba.
Pamoja
na mafanikio hayo yaliyopatikana mamlaka hiyo pia inakabiliwa na changamoto
mbalimbali, ikiwemo baadhi ya maeneo kushindwa kutumia mashine zinazotumika
kutolea risiti na kutunza kumbukumbu, kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme
kwa wafanyabiashara waishio katika maeneo ambayo hayana miundombinu hiyo
hususani vijijini.
No comments:
Post a Comment