WAZIRI wa mambo ya ndani wa
Bolivia, Carlos Romero amesema, kuwa maafisa kadhaa wa serikali wametiwa
mbaroni kwa kujaribu kupokea pesa kutoka kwa mfanyibiashara mmoja
kutoka Marekani ambaye anahudumia kifungo cha jela nchini humo.
Wale waliokamatwa ni pamoja na Mkurugenzi wa maswala ya kisheria katika wizara ya mambo ya ndani Fernando Rivera.
Mfanyibiashara huyo wa mjini New York , Jacob Ostreicher, alikamatwa mwaka uliopita kwa kosa la kuhamisha pesa nyingi bila kibali baada ya kuekeza dola milioni ishirini na tano katika biashara ya uzalishaji wa mpunga nchini Bolivia.
Amesema mashtaka dhidi yake ni hila ya kutaka kumpokonya pesa zake.(BBC News)
No comments:
Post a Comment