Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Chande Nalicho (hayupo pichani) wakati wa kikao cha baraza la madiwani hao kilichofanyika mjini humo hivi karibuni.
Na Dustan
Ndunguru,
Tunduru.
MADIWANI na
watumishi katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma, wametakiwa
kufanya kazi kwa ushirikiano na kuachana na tabia ya kuendekeza malumbano
yasiyo na tija kwa wilaya hiyo na kwa taifa kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya
hiyo Bw. Chande Nalicho alisema hayo kufuatia kuwepo kwa tofauti za kiutendaji katika
halmashauri hiyo, zilizosababisha kuwepo kwa makundi baina ya watumishi
na watumishi na baadhi ya madiwani hivyo kusababisha miradi ya maendeleo,
kutokamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Bw. Nalicho
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika mjini hapa, ambapo aliwaagiza madiwani hao kusimamia
kwa umakini miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, badala ya kusubiri taarifa za wataalamu
ambao wakati mwingine wamekuwa sio waaminifu.
Alisema ili malengo ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo yaweze kufikiwa kama ilivyokusudiwa, madiwani na watendaji wanapaswa kuwa kitu kimoja na kwamba kuendekeza migogoro hakuwezi kuleta tija.

“Serikali
imedhamiria kuwaletea watanzania maendeleo ya kweli na ndio maana ilikuja na
kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania, lakini kauli mbiu hiyo
imekutana na kikwazo cha watu wachache wanaokwamisha kwa maslahi yao binafsi”, alisema.
Aliwataka watumishi na madiwani ambao hawaelewani kumaliza tofauti zao kupitia vikao halali na kwamba ili wananchi wajenge imani na serikali miradi yote iliyobuniwa inapaswa kukamilika kwa wakati uliopangwa na kuanza kuwanufaisha wananchi hao.

Mkuu huyo wa
wilaya ya Tunduru alisema madiwani hawana budi kuacha kufika mara kwa
mara katika ofisi zao za halmahauri bila ya kuwa na sababu za msingi, kwani
kitendo hicho ndicho chanzo cha kuzalisha majungu na fitina kati yao na wataalamu.
No comments:
Post a Comment