CHAMA cha kupigania haki za
kiraia nchini Marekani kimewasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi wa
jeshi la taifa hilo, kuwapiga marufuku wanajeshi wa kike kufanya kazi
katika maeneo ya vita.
Chama hicho ambacho kiliwasilisha kesi hiyo kwa niaba ya wanajeshi wanne wa kike kinasema sera hiyo inakiuka katiba.
Kundi hilo linasema licha ya hatua ya kulegeza sera hiyo katika miaka ya hivi karibuni, wanawake bado wananyimwa fursa ya kuhudumu katika nyadhfa zaidi ya mia mbili vitani katika jeshi la Marekani.
Msemaji katika afisi ya waziri wa ulinzi, Leon Panetta, amesema kuwa takriban nyadhfa elfu kumi na tano za kivita katika jeshi la Marekani zimetolewa kwa wanawake tangu achukue hatamu za uongozi katika wizara hiyo.(BBC News)
No comments:
Post a Comment