Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
HALMASHAURI ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma, imeazimia kununua
mitambo maalum ya kusaga takataka, ili kuondokana na hatari ya kukumbwa na
magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu ikiwemo kipindupindu.
Akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani, Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri hiyo Oscar Yapesa alisema kuwa takataka hizo pia zitakuwa
zikisagwa kwenye mitambo hiyo, na kutumika kama mbolea kwenye mashamba ya
wakulima.
Oscar Yapesa. |
Kadhalika Mkurugenzi huyo alisema kwamba, wanakabiliwa na
changamoto ya gari la kuzoa taka hizo ambapo hivi sasa wanagari moja tu ambalo
halitoshelezi mahitaji halisi.
Naye Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga kwa upande wake
aliwataka Madiwani hao kuhakikisha wanawaelimisha wananchi ya juu ya utunzaji
wa mazingira, ili kuepukana na ugonjwa huo wa kipindupindu.
Kwa ujumla Halmashauri ya mji wa Mbinga, inazalisha takataka
tani 18 kwa siku na ina uwezo wa kuzoa tani tatu tu kwa siku jambo ambalo linatishia
afya za wakazi wa mji huo, wakihofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko yanayotokana
na uchafu.
No comments:
Post a Comment