Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. |
Dar es Salaam,
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Kanda, huduma kwa wateja Bohari kuu ya Dawa (MSD) hapa nchini, Cosmas
Mwaifwani (pichani juu) na wenzake watatu kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi bilioni
1.5.
Uamuzi huo wa Waziri ameutangaza leo Februari 15 mwaka huu, alipokuwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati akipokea shehena ya vitanda kutoka MSD ili
kuweka kwenye jengo lililoelekezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
libadilishwe matumizi yake kutoka kuhudumia maafisa wa Wizara ya Afya na kuwa
wodi ya wazazi kwa lengo la kupunguza msongamano.
Wengine waliosimamishwa ni pamoja na Mkurugenzi wa fedha
Joseph Tesha, Mkurugenzi wa ugavi, Misanga Muja na Mkurugenzi wa manunuzi,
Henry Mchunga.
“Wote wanne wanasimaishwa kazi kuanzia leo hii, ili kupisha
uchunguzi wa upotevu wa fedha hizi kiasi cha shilingi bilioni 1.5.”, alisema Waziri
Ummy.
No comments:
Post a Comment