Na Steven Chindiye,
Tunduru.
MVUA iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika vijiji
vya Marumba na Morandi, wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma imeezua na kubomoa nyumba
62 za wananchi na kuwaacha wakiwa hawana mahali pa kuishi.
Taarifa za tukio hilo zinafafanua kwamba mvua hiyo ilianza
kunyesha majira ya saa 10 za jioni February 6 mwaka huu, ambazo ziliambatana na
radi huku upepo mkali ukianza kuezua mapaa ya nyumba hizo.
Walisema kufuatia hali hiyo, watu waliokumbwa na adha hiyo
walianza kukimbia huku na huko wakiwa wanapita kuomba msaada wa kujihifadhi kwa
majirani na ndugu zao.
Akizungumzia tukio hilo Diwani wa kata Marumba, Msenga Said
Msenga alithibitisha uwepo wa tukio hilo na kuongeza kuwa hivi sasa wahanga
wote wamepokelewa na kuhifadhiwa na jamaa zao, katika maeneo jirani wakiwa
wanasubiri uwezekano wa kufanya ukarabati au kujenga upya nyumba zao baada ya
msimu huu wa mvua kwisha.
Alisema tukio hilo lilikuwa sio la kawaida ukilinganisha na
matukio mengine yaliyowahi kutokea katika vijiji hivyo, na kwamba awali yeye
kwa kushirikiana na viongozi wa serikali katika kata yake walitamani
kuwapeleka wahanga hao katika majengo ya shule za serikali, ili kuwahifadhi kwa
muda lakini waathirika wote walichukuliwa na kuhifadhiwa katika nyumba za
majirani na ndugu zao.
Baada ya tukio hilo na kutoa huduma za awali kwa wahanga hao kukamilika,
walipeleka taarifa kwa viongozi wa serikali ngazi ya wilaya, kwa ajili ya
kuomba msaada zaidi na kwamba tukio hilo ni la pili kwa wananchi wa vijiji
hivyo kukumbwa na mkasa wa aina hiyo ambapo, Januari mwaka mwaka huu
zaidi ya nyumba 21 ziliezuliwa na nyingine kubomolewa na mvua hizo.
No comments:
Post a Comment