Wakurugenzi na viongozi wa kutoka katika Halmashauri za mkoa
wa Ruvuma, wakishiriki semina ya kampeni ya kumeza vidonge kwa magonjwa yaliyosahaulika
mjini Songea.
|
Na Mwandishi wetu,
Songea.
WANANCHI wanaoishi katika mkoa wa Ruvuma na nje ya mkoa huo,
wametakiwa kujikinga kwa kujenga mazoea ya kumeza dawa, ambazo huzuia kuenea
kwa magonjwa yaliyosahaulika.
Imeelezwa kuwa endapo watazingatia hilo, wataweza kuepukana
na magonjwa ya matende, usubi, kichocho, trakoma na minyoo.
Mratibu wa magonjwa hayo hapa nchini, Dkt. Edward Kirundi aliyasema
hayo mjini hapa na kuongeza kuwa magonjwa hayo
yanatibika, na kwamba jambo muhimu kila mtu anapaswa kuzingatia tiba au
kinga.
Vilevile alisisitiza kwa kuitaka jamii hapa nchini, kushiriki
kikamilifu katika kampeni ya kutokomeza magonjwa hayo na wataalamu wa afya wazingatie
kutoa elimu sahihi kwa wananchi, ili kuifanya jamii iweze kuwa na uelewa juu ya
madhara yatokanayo na magonjwa hayo.
No comments:
Post a Comment