Na Kassian Nyandindi,
Songea.
BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imepongezwa kwa hatua iliyochukua ya
kufanya ukarabati wa vyoo vya wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Makambi,
iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Wanafunzi shule ya msingi Makambi, wakifurahia. |
Ukarabati huo uliofanywa, umeelezwa kuwa ni msaada mkubwa kwa
watoto hao na kwamba itasaidia waweze kuwa na vyoo bora na kuepukana na
magonjwa mbalimbali.
Shule ya msingi Makambi ina wanafunzi 850, ambapo imepata
ufadhili wa kukarabatiwa vyoo hivyo, vyenye matundu 12 kwa thamani ya shilingi
milioni 4.7.
Ofisa uhusiano wa Benki ya Posta hapa nchini, Noves Mosses
amekabidhi vyoo hivyo kwa Mwalimu mkuu msaidizi
wa shule hiyo, Kanisius Ngongi baada ya kukamilika ukarabati wake.
Wanafunzi wa shule hiyo wamefurahia kukarabatiwa kwa vyoo hivyo, ambapo awali walisema kuwa walikuwa wakitumia choo kimoja wanafunzi wengi jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwao kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali, hasa kwa watoto wa kike.

No comments:
Post a Comment