Na Yeremias Ngerangera,
Namtumbo.
WANANCHI wanaoishi katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,
wamelalamikia gharama za kusafirisha wagonjwa wao kutoka wilayani humo kwenda
hospitali ya Rufaa Songea, wakidai kuwa hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa
na uongozi wa Manispaa ya Songea mkoani humo kuzuia magari kushusha abiria
katika eneo la hospitali hiyo.
Malalamiko hayo ya wananchi hao yaliwasilishwa mbele ya Mkuu
wa mkoa huo, Dkt. Binilith Mahenge katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini
hapa juzi, huku wakiongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwatesa wananchi hao na wagonjwa
wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hiyo.
Walibainisha kuwa gharama kubwa zipo katika kukodi magari
kama vile taxi ambapo madereva wanaoendesha gari hizo huwatoza shilingi 10,000 mpaka
12,000 kutoka stendi kuu Msamala mjini Songea.
Kwa upande wake Dkt. Mahenge aliwataka wananchi hao, kuwa
watulivu wakati Ofisi yake inalifanyia kazi ili kuweza kuondoa usumbufu huo
wanaoupata sasa.
No comments:
Post a Comment