Na Kassian Nyandindi,
Songea.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma, kimeibuka na ushindi
wa kishindo baada ya wagombea wake wa nafasi za udiwani kushinda katika kata
mbili ya Tanga, iliyopo Manispaa ya Songea na Maguu wilayani Mbinga mkoani humo.
Uchaguzi huo ulifanyika Januari 22 mwaka huu ambapo katika
kata ya Maguu msimamizi wa uchaguzi huo, Caspary Mahay alimtangaza Manfred
Kahobela kuwa mshindi kupitia tiketi ya CCM baada ya kujizolea kura 2,355 na
kumbwaga chini Bahati Mbele wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
aliyepata kura 1,717.
Katika kata ya Tanga msimanizi wa uchaguzi huo, Tina Sekambo
alimtangaza Agaton Goliyama kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi kuwa mshindi
baada ya kupata kura 1,867 huku akiwashinda wagombea wa Chama cha demokrasia na
maendeleo Vinitan Soko aliyepata kura 722, ACT Wazalendo Swaiba Mapunda kura 2
na Adolf Ngonyani wa CUF aliyepata kura 15.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi Manfredy
Kahobela wa kaya ya Maguu wilayani Mbinga, aliwashukuru wananchi wa kata hiyo
kwa kukiamini CCM na kwamba atahakikisha anashirikiana nao kwa karibu katika
shughuli mbalimbali za maendeleo bila kujenga ubaguzi wa aina yoyote ile.
Naye Goliyama wa kata ya Tanga katika Manispaa ya Songea alieleza
kuwa ushindi wa Chama cha mapinduzi alioupata, umedhihirisha wazi kuwa namna
ambavyo Watanzania wanavyoendelea kukiamini chama hicho kutokana na utekelezaji
wa yale ambayo yaliahidiwa yanavyofanyika kwa vitendo na serikali ya awamu ya
tano.
No comments:
Post a Comment