Na Kassian Nyandindi,
Songea.
IMEBAINIKA kuwa jumla ya watu wazima 3,460 wanaoishi katika
Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma hawajui Kusoma, Kuandika na
Kuhesabu (KKK).
Kati ya watu hao wanaume ni 1,720 na wanawake ni 1,740 ambapo
takwimu za idadi ya watu hao ni kuanzia wenye umri wa miaka 19 hadi 65.
Albano Midelo Afisa habari Manispaa ya Songea. |
Midelo alisema kuwa licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji
wa elimu ya watu wazima hapa nchini, ameyataja mafanikio ambayo yamepatikana
katika elimu ya watu wazima katika Manispaa hiyo kuwa ni udahili wa wanafunzi
wa kidato cha kwanza umepanda toka asilimia 84.6 mwaka 2015 hadi kufikia
asilimia 98.5 mwaka 2016.
Alisema kuwa hali hiyo hutokana na utekelezaji wa elimu bila
malipo, kupanda kwa ufaulu katika mitihani ya kidato cha nne na sita na
uanzishwaji wa shule ya sekondari Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kidato cha tano
na sita.
Mafanikio mengine ni ujenzi wa hosteli ya wasichana katika
sekondari ya Matogoro na kumaliza tatizo la meza na viti vya kukali wanafunzi katika
shule za sekondari zilizopo katika Manispaa ya Songea.
Alifafanua kuwa idadi ya watu wazima wasiojua kusoma, kuandika
na kuhesabu imeendelea kuongezeka na kufikia zaidi ya watu milioni 10 kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment