Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
Aidha kufuatia hali hiyo imefanikiwa
kuokoa kiasi cha shilingi milioni 26,474,000 katika kila awamu ya uhaulishaji
fedha kwa kaya hizo maskini na wilaya imeweza kurejesha shilingi milioni
4,784,000 kutokana na walengwa hao kukosa sifa.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya
hiyo, Cosmas Nshenye alisema kuwa kufuatia kuwepo kwa tatizo hilo serikali
imechukua hatua ya kumsimamisha kazi Mratibu wa TASAF wilaya, Ahsante Luambano ambaye
anadaiwa kuzembea katika kusimamia majukumu yake ya kazi ipasavyo ili kupisha
uchunguzi.
Nshenye alisema kuwa baadaye
watakaofuatia katika zoezi hilo la kusimamishwa kazi ni watendaji wa kata na
vijiji ambao nao katika maeneo yao yaliyokuwa yakitekelezwa miradi ya mfuko huo
yataonekana kuwa na mapungufu hayo.
“Wilaya ya Mbinga inatekeleza mpango
wa kunusuru kaya maskini ili kuboresha maisha yao na kujenga uelewa kwa
wananchi wote juu ya kupiga vita umaskini, jumla ya vijiji 108 kati ya 170
vyenye wanufaika 10,307 waliwezeshwa katika mpango huu wa kunusuru kaya
maskini”, alisema Nshenye.
Vilevile Nshenye alifafanua kuwa kiasi
cha shilingi bilioni 3,574,427,206.54 kimetumika katika utekelezaji wa mpango
huo hadi Disemba mwaka jana, kati ya shilingi bilioni 3,600,955,204.57
zilizopokelewa.
Aliongeza kuwa wilaya ilifanya zoezi
la uhakiki na kubaini walengwa 191 wasiokuwa na sifa au kukosa vigezo vya
kuendelea kuwemo kwenye mpango huo ambapo miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na
mlengwa kufariki, kuhama na kwamba katika kaya kuwa mjumbe wa serikali ya
kijiji au mwenyekiti wa kitongoji katika eneo husika.
No comments:
Post a Comment