Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
Mbinga.
OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini
katika Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma, imetoa vifaa vya ujenzi kwa
shule ya msingi Mbinga vyenye thamani ya shilingi milioni 1,178,000 kwa ajili
ya kukamilisha kazi ya ujenzi wa choo cha wanafunzi wa shule hiyo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya
Mbunge wa jimbo hilo Sixtus Mapunda Katibu wa Mbunge huyo, Geddy Ndimbo alisema
kuwa vifaa walivyokabidhi wanaunga mkono nguvu za wananchi ambao walijitolea
kujenga vyoo vya matundu nane ili wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waweze
kuwa na mazingira mazuri yenye vyoo vya kisasa.
Ndimbo alifafanua kuwa shule hiyo
ambayo ipo katika kata ya Mbinga mjini B vyoo walivyokuwa wanatumia watoto hao
hapo awali, vilikuwa chakavu havifai kwa matumizi hivyo anawapongeza wananchi
waliojitokeza na kuchangia michango yao ya ujenzi huo.
Vifaa vya ujenzi walivyokabidhi ni
saruji mifuko 25, masinki nane ya vyoo, mabomba manne ya kutolea uchafu na
viungo vyake (T – Joint).
Pia aliongeza kuwa Ofisi ya Mbunge huyo
inachimba kisima cha maji shuleni hapo ambacho baadaye watajenga pampu
itakayokuwa inatoa maji kwa ajili ya matumizi ya watoto hao na walimu.
Vilevile katika kata hiyo ambayo ina
shule ya Sekondari Mbinga alisema kuwa watakabidhi tenki kubwa la kuhifadhia
maji lenye ujazo wa lita 2,000 ambalo lina thamani ya shilingi 700,000 ili
kuwawezesha wanafunzi na walimu wanaosoma katika shule hiyo waweze kuhifadhi
maji safi na salama kwa ajili ya matumizi yao mbalimbali.
Kwa upande wake diwani wa kata ya
Mbinga mjini B, Frank Mgeni amenukuliwa akitoa shukrani zake akisema, “kwa nafasi
ya pekee nimshukuru sana Mbunge wangu Sixtus na Katibu wake Geddy kwa kuniunga
mkono katika ujenzi wa choo hiki toka kinaanza kujengwa hadi leo napokea tena
vifaa vingine ambapo baada ya wiki mbili choo kitaanza kutumika,
“Niseme tu vifaa vyote vya kiwandani
vya ujenzi wa choo hiki vimetoka kwa Mbunge pekee natambua tena mchango wake wa
fedha kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji shuleni hapa”.
No comments:
Post a Comment