Na Kassian Nyandindi,
Songea.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani
Ruvuma kimeibuka kidedea kwa kuwa mshindi katika chaguzi za nafasi ya udiwani zilizofanyika
mkoani humo baada ya wagombea wake kushinda kwa kura nyingi.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari mjini hapa Katibu wa CCM mkoani humo, Amina Imbo alisema kuwa uchaguzi
huo uliofanyika ulirudiwa baada ya wagombea wake kufariki dunia.
Imbo alisema kuwa katika mkoa huo
kata ambazo uchaguzi huo ulikuwa ukifanyika ni kata ya Mhongozi iliyopo
wilayani Mbinga, Lukumbule na Kalulu zilizopo wilayani Tunduru mkoani hapa.
Katibu huyo alifafanua kuwa katika
kata hizo vyama ambayo vilishiriki uchaguzi huo na kuweka wagombea wake ni
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT
Wazalendo na Chama Cha Wananchi (CUF).
Alisema kuwa CCM katika kata ya
Mhongozi wilayani Mbinga ilimsimamisha mgombea wake, Florian komba aliyepata
kura 749, CHADEMA alikuwa Joseph Mahua alipata kura 284 na CUF Pasience Ndimbo
kwa kura 15.
Vilevile katika wilaya ya Tunduru
kata ya Lukumbule alikuwa Milepa Makande (CCM) alipata kura 1572, Omary Ghaibu
(CUF) kura 1351, Nassoro Mkopoto (CHADEMA) kura 234 na Sian Mbwana (ACT)
aliyepata kura 12.
Katika kata ya Kalulu wilayani humo
Rabii Makunga (CCM) kura 706, Kauga Hassan (CHADEMA) alipata kura 56 na Kwali
Ally (CUF) ambaye naye alipata kura 518.
Pamoja na mambo mengine, chaguzi hizo
zilifanyika baada ya kuanza mchakato wake Oktoba 15 mwaka huu na kufikia
hitimisho Novemba 26 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment