Zao la Mbaazi. |
Songea.
WAKULIMA wanaojishughulisha na kilimo
cha zao la mbaazi katika kata ya Mgazini Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani
Ruvuma wametelekeza zao hilo mashambani baada ya kukosa soko la uhakika.
Kata ya Mgazini ni kati ya maeneo ambayo
uzalishaji mkubwa wa mazao mbalimbali unafanyika ikiwemo zao hilo.
Msimu wa mwaka huu zao hilo
limekumbwa na changamoto ya kukosa soko la uhakika jambo ambalo limewafanya baadhi
ya wakulima waache kuvuna mashambani walikozalisha huku wengine wakisema hawaoni
sababu ya kuendelea kupoteza nguvu zao.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 zao
la mbaazi lilikuwa linauzwa kati ya shilingi 1,000 hadi 1,500 kwa kilo lakini
katika kipindi cha mwaka huu bei ya kilo moja ni kati ya shilingi 100 hadi 120 hivyo
wakulima wengi wamekata tamaa na kuacha mbaazi zao mashambani bila kuvuna
kutokana na kiwango hicho cha fedha kuwa kidogo na kukosa soko la uhakika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
walidai kuwa hivi sasa kutokana na hali hiyo inatishia kuongezeka kiwango cha
umaskini kwenye kaya zao huku baadhi yao walikuwa wakitegemea waweze kupata
fedha za kupeleka watoto wao shule.
Walisema zao hilo ndilo lilikuwa zao
ambalo wanategemea pia kukuza uchumi wao na kwamba wameiomba Serikali kwa kuwa
haifanyi biashara hivyo iruhusu soko huria ambalo litatoa fursa kwa mkulima kwenda
kutafuta soko lingine nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment