Na Muhidin Amri,
Mbinga.
WILAYA ya Mbinga mkoani Ruvuma, imefanikiwa kuongeza kiwango
cha akina mama wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya afya na
Hospitali, kutoka asilimia 76 mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 90 mwezi Juni
mwaka huu.
Mbali na hilo, pia kiwango cha wateja wanaotumia njia za
kisasa za uzazi wa mpango nacho kimezidi kuongezeka, kwani hivi sasa idadi ya
wazazi wanaopata huduma hiyo imefikia asilimia 105 kutoka asilimia 33, mwaka
2013 na asilimia 85 kwa mwaka 2014.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga. |
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Senyi Ngaga alipokuwa
akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya kuimarika kwa huduma ya
akina mama wajawazito wilayani humo na mkakati wa kuzuia maambukizi mapya ya Virusi
vya ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kabla na baada ya
kujifungua.
Ngaga alisema, idadi ya vifo vya watoto walio chini ya umri
wa miaka mitano vimepungua kutoka vifo 169 sawa na vifo 10/1000 mwaka
2013 hadi kufikia vifo 84 ambavyo ni sawa na vifo 7/1000 na mpango uliopo ni
kumaliza kabisa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua akina mama hao, kwani
baadhi yake vinatokana na uzembe wa mama kushindwa kuwahi hospitali mapema.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Mbinga, alibainisha kwamba wilaya
yake imefanikiwa kupunguza kiwango cha vifo vya mama wajawazito/wazazi kutoka
(11)65/100,000 mwaka 2013 hadi kufikia (8)61/100,000 mwaka 2014 hata hivyo bado
wanaendelea na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na tatizo hilo na dhamira yao
ni kupunguza, hadi kufikia wastani wa vifo (4)35/100,000.
Katika mkakati huo alisema unakwenda sambamba na suala la
kutoa elimu juu ya ukimwi, pamoja na kuwapima akina mama
wanaokwenda katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kufuata huduma
za uzazi kikamilifu, ambapo akina mama 6,810 waliojifungua, kati yao 591
waligundulika kuwa na matatizo kabla na baada ya kujifungua.
Ngaga alisema, akina mama 5,219 ambayo ni sawa na asilimia
76.6 walijifungua kwa njia ya kawaida na 1,214 walijifungua kwa njia ya
upasuaji na waliopata huduma za dharura zinazotolewa katika vituo vitano na
kati yao akina mama 6,047 waliojifungua waliingia chumba cha uzazi wakiwa
wamepimwa.
Hata hivyo alieleza kuwa mpango huo tayari kuna vituo 59,
vinavyotoa huduma ya chanjo kwa watoto na watoto 5,966 walipata chanjo ya penta
3 kati yao watoto 184 walizaliwa na akina mama wenye virusi vya ukimwi na 179
waliochukuliwa damu kwa ajili ya uchunguzi, watoto sita waligundulika kuwa na
maambukizi ya ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment