Na Steven Augustino,
Mbinga.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kimewataka madiwani na wabunge wateule kufanya kazi za kuwatumikia wananchi, ili kuondokana na tatizo la umaskini unaoendelea kutafuna wananchi wa wilaya hiyo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kimewataka madiwani na wabunge wateule kufanya kazi za kuwatumikia wananchi, ili kuondokana na tatizo la umaskini unaoendelea kutafuna wananchi wa wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa na Katibu wa CCM wa wilaya ya Mbinga, Zainabu
Chinowa alipokuwa akizungumza na viongozi hao wateule na baadhi ya wanachama wa
Chama hicho kwenye sherehe fupi ya kuwapongeza iliyofanyika ukumbi wa Mbicu hotel
uliopo mjini hapa.
Alisema yeye kama mtendaji mkuu wa chama ngazi ya wilaya, amefurahishwa
na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu kwa sababu yameonesha bado chama hicho
kinapendwa na wananchi, tofauti na baadhi ya watu wengine wanavyofikiri.
Kwa mujibu wa Katibu huyo, alisema kuwa wagombea wa CCM
wamepata ushindi ambao yeye binafsi hakutegemea kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo
hasa katika jimbo la Mbinga mjini, ambapo wagombea wa vyama vingine kama
vile NCCR Mageuzi walikuwa wakitumia ukabila kutaka kumchafua mgombea wa CCM
asiweze kupata ushindi katika uchaguzi huo.
Aliongeza kuwa hata katika nafasi ya udiwani chama hicho,
kimeweza kushinda viti vingi zaidi ikilinganishwa na vyama vingine, na kwamba jimbo
la Mbinga mjini kulikuwa na wagombea 19 wa udiwani ambapo CCM imeshinda viti 17
huku Chadema ikiambulia viti 2.
Alisema atika jimbo la Mbinga vijijini, kulikuwa na kata 29
katika matokeo ya uchaguzi huo, CCM bado kimeendelea kufanya vizuri baada
ya madiwani wake, 28 kuchaguliwa kuingia katika baraza la madiwani la mwaka 2015/2020
na CHADEMA kikipata diwani mmoja tu.
Alifafanua kuwa, hata kwa nafasi ya urais mgombea wa CCM amemshinda
kwa kura nyingi mgombea wa CHADEMA
ambapo katika kata 48 zilizopo wilayani humo, Dokta John Magufuli
ameshinda kata 47 na Edward Lowassa akiambulia ushindi katika kata moja ya
Mbinga mjini B.
Mbali na ushindi huo, mgombea udiwani wa Chama
Cha Mapinduzi katika jimbo la Mbinga mjini mwandishi wa habari
gazeti la Uhuru mkoani Ruvuma, Dastan Ndunguru aliibuka mshindi baada ya kupita
bila kupingwa katika kata ya Kihungu.
No comments:
Post a Comment