IMEANDALIWA NA MAWAKILI
WETU
( 1 )Askari
akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho
ni haki yako.
( 2 )Askari
akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama
anasema ametumwa na mahakama kukukamata, ni haki yako.
( 3 )Askari
akikukamata akwambie kwa nini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni
haki yako.
( 4
)Unaruhusiwa na ni sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama
hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
( 5 )Askari
anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni
haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari
haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa
kutii amri halali.
( 7 )Askari
haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa
halisi.
( 8 )Askari
haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
( 9 )Askari lazima
akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo
kilipotolewa, jina la mtu au sehemu ya upekuzi au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
( 11 )Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni
mpaka saa 12 asubuhi.
( 12 )Ni haki yako kumpekua askari kabla
hajakupekua ili asipandikize kitu.
( 13 )Usipekuliwe nyumbani bila kuwapo kiongozi wa
mtaa.
( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe
na askari aweke sahihi.
( 15 )Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki
salama.
( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhusiwi
kwa mwanaume.
( 17 )Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo
taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini
afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni
haki yako.
( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani
yatakuletea shida.
( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo
chini ya ulinzi.
HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO,
ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA
USIZIOMBE.
(Kwa hisani ya sheriayakub.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment