IMEANDALIWA NA MAWAKILI
WETU
( 1 ) Kama unahojiwa na Wakili mahakamani usijibu bila kutafakari alichokuuliza.
( 2 ) Wakili asikuogopeshe kwa ukali anapokuuliza
kwani ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha
ulichopanga kusema.
( 3 ) Usilazimishe kujibu kitu ambacho hukijui ni bora
kusema sijui kuliko kulazimisha kujibu.
( 4 ) Penda sana kujiamini kwakuwa kujiamini
hupunguza uwezo wa Yule anayekuuliza, hata awe Jaji/Hakimu.
( 5 ) Jitahidi kupata ushauri wa wanaojua sheria
kwa kila hatua unayopiga katika kesi.
( 6 )Kama we ni shahidi hakikisha
unajadiliana vya kutosha na Yule unayemtolea ushahidi kabla
hamjaingia mahakamani.
( 7 )Usipaniki kiasi cha kutoa neno lolote la kashfa
,kejeli, au tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa la
kuidharau mahakama.
( 8 )Katika kesi ya jinai usikubali kosa haraka kabla hujajua
kitaalam kosa hilo linaundwa na nini(vipengele vya kosa).
( 9 )Kama hukuelewa vizuri kosa
ulilosomewa ni bora kukaa kimya, kwakuwa ukikaa kimya
unaandikiwa umekataa kosa.
( 10 )Kanuni ya sheria ni kuwa, Ni kazi ya
aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa na si
kazi yako kuthibitisha kuwa haujatenda kosa.
( 11 )Katika kesi ya jinai msikilize kwa makini anayekushitaki
na hakikisha unapata lolote lenye kutia shaka katika maelezo yake na
iambie mahakama shaka hilo hii ni kwasababu huwezi kuwa na hatia kama
kuna shaka katika maelezo.
(12)Kama ulitenda kosa katika harakati za kujitetea
usidhuriwe iambie mahakama kuwa ulitenda kosa ukijilinda(self defence)
inaruhusiwa, hata kama uliua waweza kuachiwa.
( 13 )Kama ndugu yako hana akili tinmamu na ametenda kosa
iambie mahakama.Hii ni kwasababu kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga
inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya wasio na akili.
( 14 )Inakubalika na ukaachiwa huru ukisema kuwa
ulilazimishwa kutenda kosa kama kweli ulilazimishwa.
( 15 )Inakubalika na ukaachiwa huru kusema kuwa
sikuwa eneo la tukio wakati likitokea kama kweli haukuwapo.
( 16 )Kama kosa ni kupita taa nyekundu ikiwaka
barabarani,swali lako kwa shahidi traffic lilenge kumbana
kama sehemu aliyokuwa amesimama alikuwa na uwezo wa kuangalia vizuri na
kutambua rangi za taa. Mfn. jua kali linawaka yeye ameuonaje mwanga wa
taa kutoka mbali.
( 17 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi muhoji maswali
mafupi. Mfn. ulikaa upande wa pili barabara, si ndio, jua kali lilikuwa
linawaka , si ndio, ulifanya kazi ya kuangalia magari mengine pia si ndio, na
mbele kulikuwa na miti si ndio, sasa kama hali ilikuwa hivyo uliwezaje kuona
taa nyekundu ikiwaka wakati nakatiza.
18 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi wako uliyemleta katu
usimuulize swali ambalo mlikuwa hamjalijadili na hivyo hujui atatoa jibu gani.
( 19 )Kama wanaokushtaki wanashahidi na unamjua kuwa
kuna kipindi aliwahi kuchangnyikiwa au kufanya tukio lolote la uhalifu
kabla, ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake mpaka aaminike
kwa anayoyatolea ushahidi leo .....Itaendelea..........
(Kwa
hisani ya sheriayakub.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment