Na Steven
Augustino,
Tunduru.
WATU watatu wamefariki dunia katika ajali ya pikipiki, baada
ya kugonga mtambo wa kujenga barabara (ROLA) ambao ni mali ya kampuni ya Sino
Hydro inayojenga barabara kwa kiwango cha lami, kutoka Tunduru mjini kuelekea
katika tarafa ya Nakapanya wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma.
Mashuda wa tukio hilo, walisema kuwa ajali hiyo
ilitokea katika kijiji cha Muhuwesi wilayani humo ambapo Diwani wa kata ya
Muhuwesi, Nurdini Mnolela aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ajali hiyo
ilitokea Novemba 15 mwaka huu wakati watu hao wakiwa wanatokea kijiji cha Majimaji
kurejea kijijini kwao Muhuwesi.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, wa pikipiki waliyokuwa
wakiendesha ambayo ni aina ya Sunlg yenye namba za usajili T 317 CUC mali ya marehemu Ahamad Athuman (30) hali ambayo,
ilimfanya ashindwe kuimudu na hatimaye kugonga mtambo huo.
Katika tuko hilo diwani huyo alisema, marehemu alikuwa amewabeba
abiria wawili ambao wote nao walifariki dunia katika eneo la tukio ilipotokea ajali
hiyo.
Mganga aliyefanyia uchunguzi miili ya marehemu hao, Dokta
George Chiwangu alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo kilisababisha na kutokwa
damu nyingi baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Chiwangu alibainisha kuwa katika ajali hiyo marehemu wote, walipata
majeraha vichwani jambo ambalo lilisababisha kupasuka vichwa vyao na ubongo
kuvurugika.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Mihayo Msikhela alithibitisha
kuwepo kwa ajali hiyo na kuwatahadharisha madereva wa vyombo vya moto kuwa
makini pindi wanapopita katika barabara, ambazo bado zipo katika matengenezo.
Hata hivyo alisema endapo kama hawatakuwa makini, wakati
wanapoendesha vyombo hivyo, ipo hatari vijana wengi kuendelea kupoteza maisha
na wengine kuwa walemavu wa maisha.
No comments:
Post a Comment