Na Kassian Nyandindi,
Songea.
HENRY Millinga (34) ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari
Msamala katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, amefariki dunia na mwili wake
ukiwa umetupwa
ana mjini Songea na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa
mkoa huo, Mihayo Msikhela zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novembkwenye
mtaro wa maji machafu.
Katika tukio hilo imeelezwa kuwa pembeni ya mwili wa mwalimu
huyo, amekutwa akiwa na vipande vya chupa za bia, huku katika paji lake la uso
akiwa na majeraha makubwa.
Inadaiwa siku ya tukio hilo, Mkuu wa Polisi wilaya ya Songea
alipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba huko katika eneo la Nane nane
Msamala kuna mtu mmoja ameonekana akiwa ametupwa katika mtaro wa maji machafu
na amepoteza fahamu, ndipo jitihada za Polisi kufika eneo la tukio zilifanikiwa
na baadaye kwenda katika eneo hilo kumkuta mtu huyo akiwa ndani ya mtaro huo amefariki.
Kamanda Msikhela alieleza kuwa askari Polisi wakiwa kwenye
eneo la tukio, huku umati mkubwa wa watu wakijitokeza kushuhudia ndipo baadhi
yao waligundua kuwa mwili wa marehemu huyo, ni mwalimu wa shule ya sekondari Msamala.
Baada ya kubaini hilo alitafutwa Mkuu wa shule hiyo ya sekondari,
Irine Chitinde ambaye alithibitisha kuwa ni mwalimu mwenzake Henry Milinga,
mkazi wa eneo moja maarufu la kwa Gasa katika Manispaa ya Songea.
Polisi walifanya jitihada ya kuuchukua mwili wake, na kuupeleka
Hospitali ya serikali ya rufaa mkoa wa Ruvuma iliyopo katika Manispaa hiyo,
ambako ilithibitishwa kuwa Milinga alikuwa ameshafariki dunia kutokana na
kuvuja kwa damu nyingi katika jeraha alilokuwa nalo kwenye paji la uso.
Uchunguzi wa awali Polisi imebaini Milinga katika uhai wake,
alikuwa akipendelea kunywa katika baa moja maarufu ya Mtini iliyopo mjini hapa na
kwamba inahofiwa kuwa mauti yalimkuta wakati akiwa anarudi nyumbani kwake, na Polisi
bado inaendelea kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha kifo chake.
No comments:
Post a Comment