Na Steven Augustino,
Tunduru.
MTU mmoja amefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa vibaya wilayani
Tunduru mkoa wa Ruvuma, kufuatia ajali iliyohusisha basi la kampuni ya, Asante
Raby lenye namba za usajili T 136 AVA na Lory la kampuni ya Sinohydro ambayo
inajenga barabara kwa kiwango cha lami wilayani humo.
Mihayo Msikhela. |
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha tukio hilo,
kilisababishwa na dereva wa Lory aina ya Steya lenye namba za usajili T 368 BUU
kuzuia basi hilo wakati likitaka kupita, ambapo baada ya ajali kutokea
alikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumzia tukio hilo wakati alipowatembelea majeruhi hao
na kuwapa pole, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela alimtaja
aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuywa ni, Khatib Juma Paswele (35) ambaye
ni mkazi wa mjini hapa.
Msikhela alifafanua kuwa katika ajali hiyo pia watu 11
walijeruhiwa kati yao 6 walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea majumbani
kwao, watano wamelazwa Hospitali ya wilaya Tunduru kwa matibabu zaidi kutokana
na kuumia vibaya, sehemu mbalimbali za miili yao.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo,
Dokta Gaofrid Mvile alithibitisha kuwapokea majeruhi hao, November 9 mwaka huu na
kuwahudumia kwa lengo la kuokoa maisha yao.
Kati ya majeruhi hao watano waliolazwa na majeruhi watatu,
bado wapo katika hali mbaya na kwamba taratibu zinafanyika kwa ajili ya
kuwapeleka Hospitali ya Ndanda, kwa matibabu zaidi kutokana na baadhi yao
kuvunjika miguu na wengine kujeruhiwa katika paji la uso.
No comments:
Post a Comment