Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhi leo orodha ya makontena yaliyopotea bandarini na ambayo TRA haina taarifa zake. |
Na Mwandishi wetu,
Dar es Salaam.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim
Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa Maofisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato hapa
nchini (TRA) na wengine kufukuzwa kazi, baada ya kufanya ziara ya kushitukiza
bandarini Jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Waziri Mkuu, imefuatia baada ya
kukuta madudu ambayo hakuyafurahia na yanadaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji
wa TRA.
Maofisa hao ambao majina yao yamehifadhiwa, ili Jeshi la
Polisi lianze kazi ya kuwashughulikia wametakiwa pia kusalimisha hati zao za
usafiri.
Utekelezaji huo umekuja baada ya kubainika kwamba, kuna
makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya
bandari (TPA) inazo, lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
No comments:
Post a Comment