Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
KAMPENI za chini kwa chini zinaendelea kufukuta katika Jimbo
la Mbinga mjini, wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, ambazo zinalenga kumpata
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Mbinga atakayeweza kuendesha baraza la
madiwani la halmashauri hiyo.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini
kuwa, baadhi ya Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba
25 mwaka huu wameanza kuvutana hapa na pale, juu ya kumpata mwenzao atakayeweza
kuendesha gurudumu hilo katika baraza lao.
Vikao vya siri vimekuwa vikifanyika katika maeneo mbalimbali,
ambapo baraza hilo kwa kiasi kikubwa lina madiwani wengi, ambao ni wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Halmashauri ya mji huo imeundwa na kata 19 ambapo katika kata
hizo, mbili zinaongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa
nafasi hiyo ya udiwani.
Duru za kisiasa ambazo zimetufikia mezani na kuthibitishwa na
vyanzo mbalimbali vya habari zinayataja majina mawili, (ambayo tunayo) yanavutana
kutaka kushika nafasi hiyo ya uenyekiti.
Hata hivyo nimezungumza na wadau wa mambo ya kisiasa wilayani
Mbinga, walisema kwa nyakati tofauti kwamba licha ya kuwepo kwa mvutano huo,
bado kuna madiwani wengine ambao watajitokeza baadaye kuchukua fomu ya
kugombea nafasi hiyo, huku wakiongeza kuwa hawataki kujitokeza sasa ni mapema mno.
…………. itaendelea
wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment