Saturday, February 9, 2013

DC TUNDURU AAHIDI KUFUNDISHA HESABU


Na Steven Augustino,
Tunduru.

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Chande Nalicho ameahidi kuingia darasani na kuanza kufundisha somo la Hisabati katika shule ya sekondari ya kutwa ya Frenki Weston,  ikiwa ni juhudi za kuhakikisha  taalunma inaongezeka kwa wanafunzi katika shule hiyo.

Sambamba na taarifa hiyo ambayo alisema kuwa ni kupunguza ikama ya upungufu wa wafanyakazi wa idara ya elimu, pia ameahidi kuanzisha utaratibu wa kufanya ziara za kushitukiza katika shule zote wilayani humo ili kujionea hali halisi ya utendaji kazi ya walimu, ambao wanadaiwa kulegalega na kusababisha wilaya yake kufanya vibaya katika matokeo ya wanafuzi waliofanya mtihani wa kumaliza daraza la saba mwaka 2012.

Nalicho aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kutathimini hali ya maendeleo ya elimu wilayani Tunduru, Wilaya uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha walimu (Klasta) mjini hapa huku akiongeza kuwa maamuzi ya kushika chaki na kuanza kufundisha yametokana na msukumo wa kusikitishwa na matokeo mabaya ya mtihani wa darasa la saba ingawa wanafunzi walitumia mfumo mpya wa kujibu maswa kwa kuchagua majibu.


“Taaluma yangu ni mwalimu mzuri tena wa hesabu naahidi kuanza kushika chaki na kufundisha  kwa lengo la konesha mfano wa uwajibikaji kwa walimu wote wilayani hapa”, alisema Nalicho.

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa kila shule kujiwekea malengo ya ufundishaji angalau kwa asilimia 60 pamoja na kuchukuliwa kwa hatua kwa wote watakaobainika, kudandanya katika matokeo ya mitihani ya kujipima ikiwa ni juhudi ya kuhakikisha kuwa wilaya ya Tunduru inapiga hatua kitaaluma katika matokeo ya mwaka 2013/2014.  

Awali kaimu afisa elimu ya shule za msingi wilayani humo Flavian Nchimbi akizungumzia taarifa za ufaulu huo alimweleza mkuu wa wilaya hiyo kuwa jumla ya wanafunzi 2788 kati yao wakiwemo wavulana 1611 na wasichana 1177 sawa na asilimia 42.3 kuwa ndio waliofanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba wilayani humo.

No comments: